Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 9.10
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha Bwana akanena na Musa katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia,Nombres 1.1 Exode 40.2
2 Tena, wana wa Israeli na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa.Lévitique 23.5 Deutéronome 16.1-16.2 Luc 22.7 2 Chroniques 35.1 Marc 14.12
3 Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaishika kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoishika.Exode 12.6-12.11 2 Chroniques 30.2 Hébreux 9.26 Nombres 9.11-9.12 Lévitique 23.5
4 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waishike sikukuu hiyo ya Pasaka; 5 Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.Josué 5.10 Hébreux 3.5 Exode 12.1-12.13 Genèse 7.5 Nombres 29.40
6 Basi walikuwako watu waume kadha wa kadha waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,Exode 18.15 Nombres 27.2 Nombres 19.11 Nombres 5.2 Nombres 19.16
7 Sisi tu hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea Bwana matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?Deutéronome 16.2 2 Chroniques 30.17-30.19 1 Corinthiens 5.7-5.8 Nombres 9.2 Exode 12.27
8 Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza Bwana atakaloagiza juu yenu.Psaumes 85.8 Nombres 27.5 Psaumes 25.14 2 Chroniques 20.17 Exode 14.13
9 Bwana akanena na Musa, akamwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa Bwana;Matthieu 5.24 1 Corinthiens 6.9-6.11 Ephésiens 2.12-2.13 Romains 16.25-16.26 Nombres 9.6-9.7
11 mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;2 Chroniques 30.2-30.15 Deutéronome 16.3 Jean 19.36 Nombres 9.3 Exode 12.2-12.14
12 wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.Exode 12.10 Exode 12.46 Jean 19.36 Exode 12.43 Nombres 9.3
13 Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake; kwa sababu hakumtolea Bwana matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake.Exode 12.15 Genèse 17.14 Nombres 5.31 Nombres 9.7 Hébreux 6.6
14 Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa Bwana; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.Exode 12.48-12.49 Lévitique 24.22 Esaïe 56.3-56.7 Lévitique 19.10 Deutéronome 31.12
15 Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi.Exode 13.21 Exode 40.34 Néhémie 9.19 Psaumes 78.14 Nombres 14.14
16 Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku.Néhémie 9.12 Deutéronome 1.33 Psaumes 78.14 1 Corinthiens 10.1 Psaumes 105.39
17 Na kila lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao.Exode 40.36-40.38 Nombres 10.33-10.34 Psaumes 32.8 Jean 10.3-10.5 Exode 33.14-33.15
18 Kwa amri ya Bwana Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya Bwana walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.1 Corinthiens 10.1 Exode 17.1 Nombres 10.13 2 Jean 1.6 Nombres 9.20
19 Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya Bwana, wala hawakusafiri.Nombres 1.52-1.53 Nombres 3.8 Zacharie 3.7
20 Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya Bwana walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya Bwana walisafiri. 21 Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.Néhémie 9.12 Néhémie 9.19
22 Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;Exode 40.36-40.37 Psaumes 32.8 Psaumes 73.24 Deutéronome 2.3-2.4 Deutéronome 1.6-1.7
23 bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya Bwana walipiga kambi yao, na kwa amri ya Bwana walisafiri; wakayalinda malinzi ya Bwana, kwa mkono wa Musa.Nombres 9.19 Ezéchiel 44.8 Zacharie 3.7 Josué 22.3 Genèse 26.5

Cette Bible est dans le domaine public.