Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Pierre 2.5
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.2 Pierre 2.3 Jude 1.4 Matthieu 7.15 Galates 2.4 1 Corinthiens 11.19
2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.Romains 2.24 Apocalypse 13.14 Jude 1.15 2 Pierre 2.15 Actes 16.17
3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.2 Corinthiens 2.17 1 Thessaloniciens 2.5 Romains 16.18 Deutéronome 32.35 1 Timothée 6.5
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;Jude 1.6 Matthieu 25.41 Esaïe 14.12 Apocalypse 20.1-20.3 Apocalypse 12.7-12.9
5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;2 Pierre 3.6 Hébreux 11.7 Jude 1.14-1.15 Matthieu 24.37-24.39 Genèse 6.1-6.8
6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;Jude 1.7 Nombres 26.10 Deutéronome 29.23 Genèse 19.24-19.25 1 Corinthiens 10.11
7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;Genèse 19.16 Genèse 19.29 1 Corinthiens 10.13 Genèse 19.7-19.8 Genèse 13.13
8 maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;Psaumes 119.158 Proverbes 25.26 Ezéchiel 9.4 Psaumes 119.136 Psaumes 119.139
9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;1 Corinthiens 10.13 Psaumes 34.15-34.19 2 Pierre 3.7 Jude 1.14-1.15 Apocalypse 3.10
10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.Exode 22.28 Jude 1.16 Jude 1.10 Luc 19.14 Romains 1.24-1.27
11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana.Jude 1.9 Psaumes 104.4 Psaumes 103.20 2 Thessaloniciens 1.7 Daniel 6.22
12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;Jude 1.10 Jérémie 12.3 2 Pierre 2.19 Jérémie 10.8 Jérémie 4.22
13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;Romains 13.13 Romains 2.8-2.9 1 Pierre 4.4 Jude 1.12-1.16 Esaïe 3.11
14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;Ephésiens 2.3 2 Pierre 2.3 2 Pierre 2.18 1 Jean 2.16 2 Pierre 3.16
15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;Jude 1.11 Apocalypse 2.14 Nombres 22.5-22.7 Deutéronome 23.4-23.5 2 Pierre 2.13
16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.Nombres 22.21-22.33 Ecclésiaste 9.3 Actes 26.24-26.25 Osée 9.7 Ecclésiaste 7.25
17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.Jude 1.12-1.13 Jérémie 14.3 Jude 1.6 Matthieu 22.13 Ephésiens 4.14
18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;2 Pierre 1.4 2 Pierre 2.20 Jude 1.15-1.16 Apocalypse 13.5-13.6 Apocalypse 13.11
19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.Jean 8.34 Galates 5.13 Galates 5.1 1 Pierre 2.16 Romains 6.12-6.14
20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.Hébreux 10.26-10.27 Hébreux 6.4-6.8 Philippiens 3.19 2 Pierre 2.18 Deutéronome 32.29
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.Ezéchiel 18.24 Hébreux 6.4-6.6 Luc 12.47 Ezéchiel 3.20 Jean 9.41
22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.Proverbes 26.11

Cette Bible est dans le domaine public.