Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 23.11
Bible en Swahili de l’est


1 Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;2 Samuel 7.8-7.9 1 Samuel 16.12-16.13 Psaumes 89.20 Psaumes 78.70-78.71 Jacques 5.13
2 Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu.2 Pierre 1.21 Matthieu 22.43 Hébreux 3.7-3.8 Marc 12.36 Actes 2.25-2.31
3 Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu,2 Samuel 22.32 Deutéronome 32.4 2 Samuel 22.2-22.3 Exode 18.21 Psaumes 110.2
4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu.Juges 5.31 Proverbes 4.18 Osée 6.5 Psaumes 72.6 Psaumes 89.36
5 Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za Bwana? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.Esaïe 55.3 Esaïe 9.6-9.7 2 Samuel 7.14-7.16 Hébreux 13.20 Esaïe 61.8
6 Lakini hatawachipuza watu wa ubatili; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Ambayo haivuniki kwa mkono,Deutéronome 13.13 Cantique 2.2 Esaïe 33.12 Matthieu 13.41 Genèse 3.18
7 Mtu atakayeigusa hiyo, Na awe na chuma na mpini wa mkuki, Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.Hébreux 6.8 Jean 15.6 Matthieu 3.10-3.12 Esaïe 27.4 Luc 19.14
8 Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni,mkuu wa maakida ;huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.1 Chroniques 27.2 1 Chroniques 11.11-11.47 1 Chroniques 27.32
9 Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;1 Chroniques 27.4 1 Samuel 17.26 Marc 14.50 1 Samuel 17.10 1 Chroniques 11.12-11.14
10 huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.1 Samuel 19.5 1 Samuel 11.13 2 Rois 5.1 Esaïe 53.12 Juges 15.18
11 Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti;2 Samuel 23.33 1 Chroniques 11.27 1 Chroniques 11.13-11.14
12 ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu.2 Samuel 23.10 Psaumes 3.8 Proverbes 21.31 Psaumes 44.2
13 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.2 Samuel 5.18 1 Samuel 22.1 Josué 15.35 1 Chroniques 14.9 Josué 12.15
14 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu.1 Samuel 22.4-22.5 1 Samuel 13.23-14.1 1 Chroniques 12.16 1 Samuel 22.1 1 Samuel 10.5
15 Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!Jean 4.14 Esaïe 44.3 Jean 4.10 Psaumes 63.1 Nombres 11.4-11.5
16 Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.Genèse 35.14 1 Samuel 7.6 1 Samuel 19.5 2 Corinthiens 5.14 Philippiens 2.17
17 Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.Lévitique 17.10 1 Samuel 2.30 1 Rois 21.3 1 Samuel 26.11 Genèse 9.4
18 Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.2 Samuel 10.10 2 Samuel 10.14 1 Chroniques 11.20-11.21 2 Samuel 18.2 2 Samuel 2.18
19 Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.2 Samuel 23.13 1 Corinthiens 15.41 2 Samuel 23.9 1 Chroniques 11.25 2 Samuel 23.16
20 Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji.2 Samuel 20.23 Josué 15.21 2 Samuel 8.18 1 Chroniques 11.22-11.24 1 Rois 1.8
21 huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.1 Samuel 17.51 1 Chroniques 11.23 Colossiens 2.15
22 Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 23 Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.1 Samuel 22.14 2 Samuel 8.8 2 Samuel 20.23 1 Chroniques 27.6
24 Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu;2 Samuel 2.18 1 Chroniques 27.7 1 Chroniques 11.26
25 na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi;1 Chroniques 11.27-11.28 Juges 7.1
26 na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi;2 Samuel 14.2 1 Chroniques 11.27-11.28 1 Chroniques 27.9-27.10
27 na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi;Josué 21.18 1 Chroniques 27.12 1 Chroniques 11.19 1 Chroniques 11.28
28 na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi;2 Rois 25.23 1 Chroniques 27.13 1 Chroniques 11.30
29 na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;1 Chroniques 11.30-11.31 Josué 18.28 1 Chroniques 27.15
30 na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi;Juges 12.15 Juges 2.9 Josué 24.30 Juges 12.13 1 Chroniques 27.14
31 na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi;2 Samuel 3.16 1 Chroniques 11.32-11.33
32 na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani,1 Chroniques 11.34
33 mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari;1 Chroniques 11.27 2 Samuel 23.11 1 Chroniques 11.35
34 na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;2 Samuel 11.3 2 Samuel 15.12 2 Samuel 15.31 1 Chroniques 27.33-27.34 2 Samuel 10.8
35 na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi;1 Chroniques 11.37 Josué 15.55
36 na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi;1 Chroniques 11.38 2 Samuel 8.3
37 na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya;1 Chroniques 11.37 2 Samuel 4.2 1 Chroniques 11.39
38 na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri;1 Chroniques 2.53 2 Samuel 20.26 1 Chroniques 11.40
39 na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba.2 Samuel 11.3 1 Chroniques 11.41 1 Rois 15.5 2 Samuel 12.9 Matthieu 1.6

Cette Bible est dans le domaine public.