Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Accueil  /  Bible  /  Bible en Swahili de l’est  / Job 8     

Job 8
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema, Job 2.11
2 Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? Job 6.26 1 Rois 19.11 Job 15.2 Job 7.11 Proverbes 1.22
3 Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? 2 Chroniques 19.7 Deutéronome 32.4 Genèse 18.25 Apocalypse 16.7 Daniel 9.14
4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Job 1.5 Job 1.18-1.19 Job 18.16-18.19 Genèse 19.13-19.25 Genèse 13.13
5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Job 11.13 Jacques 4.7-4.10 Hébreux 3.7-3.8 Matthieu 7.7-7.8 2 Chroniques 33.12-33.13
6 Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Psaumes 7.6 1 Jean 3.19-3.22 Job 21.14-21.15 Psaumes 59.4-59.5 Esaïe 1.15
7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. Job 42.12-42.13 Matthieu 13.31-13.32 Zacharie 4.10 Proverbes 4.18 Zacharie 14.7
8 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; Job 15.18 Deutéronome 4.32 Deutéronome 32.7 Esaïe 38.19 Job 32.6-32.7
9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) 1 Chroniques 29.15 Job 14.2 Psaumes 144.4 Job 7.6 Psaumes 102.11
10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? Job 32.7 Deutéronome 11.19 Psaumes 145.4 Matthieu 12.35 Hébreux 12.1
11 Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? Esaïe 19.5-19.7 Exode 2.3
12 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. Jérémie 17.6 Psaumes 129.6-129.7 1 Pierre 1.24 Matthieu 13.20 Jacques 1.10-1.11
13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia; Psaumes 9.17 Job 13.16 Job 11.20 Job 15.34 Proverbes 10.28
14 Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui. Esaïe 59.5-59.6
15 Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu. Job 27.18 Matthieu 7.24-7.27 Luc 6.47-6.49 Psaumes 112.10 Psaumes 49.11
16 Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake. Psaumes 80.11 Psaumes 73.3-73.12 Jérémie 11.16 Psaumes 37.35-37.36 Job 5.3
17 Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe. Jude 1.12 Esaïe 5.24 Marc 11.20 Job 29.19 Esaïe 40.24
18 Lakini, aking’olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona. Job 7.10 Psaumes 37.36 Job 7.8 Psaumes 37.10 Job 20.9
19 Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi. Job 20.5 1 Samuel 2.8 Psaumes 113.7 Matthieu 3.9 Psaumes 75.7
20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. Job 4.7 Psaumes 37.37 Psaumes 37.24 Esaïe 45.1 Job 9.22
21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. Psaumes 126.2 Genèse 21.6 Psaumes 100.1 Psaumes 32.11 Psaumes 126.6
22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena. Psaumes 132.18 Psaumes 109.29 Psaumes 35.26 Job 8.18 Job 18.14

Cette Bible est dans le domaine public.