Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 73.12
Bible en Swahili de l’est


1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.Matthieu 5.8 Luc 12.32 Psaumes 84.11 Psaumes 50.1 Jean 1.47
2 Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.Psaumes 94.18 1 Samuel 2.9 Psaumes 38.16 Psaumes 17.15 Psaumes 17.5
3 Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.Job 21.7 Jérémie 12.1 Psaumes 37.1 Psaumes 37.7 Proverbes 23.17
4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na mwili wao una nguvu.Job 24.20 Ecclésiaste 2.16 Psaumes 17.14 Ecclésiaste 7.15 Luc 16.22
5 Katika taabu ya watu hawamo, Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.Psaumes 73.12 Job 21.9 Jérémie 12.1-12.2 Job 21.6 1 Corinthiens 11.32
6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Jeuri huwavika kama nguo.Psaumes 109.18 Juges 8.26 Proverbes 1.9 Jacques 5.4-5.6 Jérémie 48.29
7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.Psaumes 17.10 Job 15.27 Jérémie 5.28 Psaumes 17.14 1 Samuel 25.36
8 Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.Jude 1.16 Psaumes 53.1-53.4 Jérémie 7.9-7.11 Psaumes 10.10-10.11 Psaumes 12.4-12.5
9 Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.Apocalypse 13.6 Jacques 3.6 2 Chroniques 32.15 Luc 18.4 Exode 5.2
10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao.Psaumes 75.8
11 Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?Ezéchiel 8.12 Job 22.13-22.14 Psaumes 94.7 Psaumes 73.9 Psaumes 44.21
12 Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.Psaumes 52.7 Jacques 5.1-5.3 Osée 12.7-12.8 Psaumes 49.6 Jérémie 5.28
13 Hakika nimejisafisha moyo wangu bure, Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.Psaumes 26.6 Job 34.9 Job 21.15 Job 35.3 Job 9.31
14 Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi.Hébreux 12.5 Job 10.17 Job 7.18 1 Pierre 1.6 Amos 3.2
15 Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.Matthieu 18.6-18.7 Malachie 2.8 Psaumes 14.5 Psaumes 22.30 Psaumes 24.6
16 Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu;Ecclésiaste 8.17 Jean 16.18-16.19 Proverbes 30.2-30.3 Psaumes 77.19 Luc 18.32-18.34
17 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, Nikautafakari mwisho wao.Psaumes 77.13 Psaumes 27.4 Luc 12.20 Psaumes 63.2 Ecclésiaste 8.12-8.13
18 Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, Huwaangusha mpaka palipoharibika.Psaumes 35.6 Deutéronome 32.35 Psaumes 37.24 Psaumes 94.23 Psaumes 92.7
19 Namna gani wamekuwa ukiwa mara! Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.Nombres 16.21 Psaumes 58.9 Job 18.11 1 Samuel 28.20 Esaïe 47.11
20 Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao.Psaumes 78.65 Job 20.8 Psaumes 39.6 Esaïe 29.7-29.8 Psaumes 90.5
21 Moyo wangu ulipoona uchungu, Viuno vyangu viliponichoma,Psaumes 37.1 Job 16.13 Psaumes 37.7 Lamentations 3.13 Psaumes 73.3
22 Nalikuwa kama mjinga, sijui neno; Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.Ecclésiaste 3.18 Psaumes 92.6 Psaumes 49.10 Proverbes 30.2 Psaumes 32.9
23 Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume.Esaïe 41.13 Psaumes 63.8 Psaumes 23.4 Psaumes 16.8 Psaumes 139.1-139.12
24 Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.Psaumes 32.8 Psaumes 48.14 Psaumes 49.15 Esaïe 58.11 Jean 17.5
25 Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.Philippiens 3.8 Psaumes 63.3 Matthieu 5.8 Psaumes 16.5 Psaumes 16.2
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.Psaumes 18.2 Psaumes 84.2 Psaumes 40.12 Psaumes 16.5-16.6 Esaïe 40.29-40.31
27 Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.Psaumes 119.155 Exode 34.15 Nombres 15.39 Jacques 4.4 Apocalypse 17.1-17.5
28 Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.Jacques 4.8 Psaumes 65.4 Psaumes 118.17 Hébreux 10.19-10.22 Psaumes 107.22

Cette Bible est dans le domaine public.