Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 11
Bible en Swahili de l’est


1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Proverbes 16.11 Proverbes 20.10 Proverbes 20.23 Deutéronome 25.13-25.16 Lévitique 19.35-19.36
2 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Luc 18.14 Proverbes 15.33 Proverbes 29.23 Proverbes 16.18-16.19 Luc 14.8-14.11
3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Proverbes 13.6 Proverbes 19.3 Proverbes 21.7 Proverbes 11.5 Proverbes 28.18
4 Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Sophonie 1.18 Proverbes 10.2 Genèse 7.1 Ezéchiel 7.19 Psaumes 49.6-49.8
5 Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Proverbes 5.22 Proverbes 1.31-1.32 Psaumes 9.15-9.16 Matthieu 27.4-27.5 Proverbes 3.6
6 Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Ecclésiaste 10.8 Psaumes 7.15-7.16 Proverbes 5.22 1 Rois 2.44 1 Samuel 12.3-12.4
7 Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Proverbes 10.28 Job 8.13-8.14 Proverbes 14.32 Exode 15.9-15.10 Job 11.20
8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Proverbes 21.18 Esther 7.9-7.10 Esaïe 43.3-43.4 Daniel 6.23-6.24
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Psaumes 55.12 Proverbes 2.10-2.16 1 Rois 22.20-22.23 1 Rois 13.18-13.22 Matthieu 15.5-15.14
10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. Proverbes 28.12 Juges 5.31 Exode 15.21 Job 27.23 Esther 8.15-8.16
11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Proverbes 29.8 Proverbes 14.34 Esther 9.1-9.16 Esther 3.8-3.15 Genèse 41.38-41.42
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Proverbes 14.21 Juges 9.27-9.29 1 Samuel 10.27 Luc 18.9 1 Pierre 2.23
13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Proverbes 20.19 Lévitique 19.16 Josué 2.14 1 Timothée 5.13 Jérémie 38.27
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Proverbes 15.22 Proverbes 24.6 Proverbes 20.18 Actes 15.6-15.21 Proverbes 16.22
15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama. Proverbes 17.18 Proverbes 20.16 Proverbes 6.1-6.5 Proverbes 22.26-22.27
16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. 1 Samuel 25.32-25.33 Proverbes 31.30-31.31 Luc 8.3 Luc 11.21-11.22 2 Jean 1.1
17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Matthieu 5.7 Matthieu 25.34-25.40 Proverbes 15.27 Matthieu 6.14-6.15 Psaumes 41.1-41.4
18 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. Jacques 3.18 Osée 10.12-10.13 Galates 6.8-6.9 Ecclésiaste 10.8 Psaumes 126.5-126.6
19 Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. Proverbes 10.16 Proverbes 19.23 Proverbes 12.28 Romains 2.8-2.9 Proverbes 7.22-7.23
20 Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa Bwana; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. Psaumes 119.1 1 Chroniques 29.17 Proverbes 12.22 Proverbes 6.14 Proverbes 13.6
21 Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. Proverbes 16.5 Actes 2.39 Jérémie 32.39 Psaumes 112.1-112.2 Proverbes 13.22
22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili. Proverbes 31.30 Genèse 24.47 Proverbes 9.13 Nahum 3.4-3.6 Ezéchiel 16.15-16.22
23 Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Romains 2.8-2.9 Proverbes 10.28 Psaumes 39.7-39.8 Jérémie 17.16 Esaïe 26.9
24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Proverbes 19.17 2 Corinthiens 9.5-9.11 Psaumes 112.9 Luc 6.38 Ecclésiaste 11.1-11.2
25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Matthieu 5.7 2 Corinthiens 9.6-9.9 Proverbes 28.27 Esaïe 58.7-58.11 Esaïe 32.8
26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Job 29.13 Genèse 42.6 Proverbes 24.24 Amos 8.4-8.6
27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Esther 7.10 Psaumes 7.15-7.16 Psaumes 57.6 Psaumes 9.15-9.16 Proverbes 17.11
28 Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Jérémie 17.8 Psaumes 1.3 1 Timothée 6.17 Job 31.24-31.25 Psaumes 92.12-92.14
29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Ecclésiaste 5.16 Proverbes 14.19 1 Samuel 25.38 1 Samuel 25.3 Osée 8.7
30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. Jacques 5.20 Daniel 12.3 Proverbes 3.18 Proverbes 15.4 Jean 4.36
31 Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi? Jérémie 25.29 1 Rois 13.24 Proverbes 13.21 1 Corinthiens 11.30-11.32 2 Samuel 12.9-12.12

Cette Bible est dans le domaine public.