Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 11.2
Bible en Swahili de l’est


1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.Proverbes 16.11 Proverbes 20.10 Proverbes 20.23 Deutéronome 25.13-25.16 Lévitique 19.35-19.36
2 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.Luc 18.14 Proverbes 16.18-16.19 Luc 14.8-14.11 Proverbes 15.33 Proverbes 29.23
3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.Proverbes 13.6 Psaumes 26.1 Psaumes 25.21 Esaïe 1.28 Ecclésiaste 7.17
4 Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti.Genèse 7.1 Sophonie 1.18 Proverbes 10.2 Ezéchiel 7.19 Romains 5.17
5 Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.Proverbes 5.22 Matthieu 27.4-27.5 Proverbes 3.6 2 Samuel 17.23 Proverbes 11.3
6 Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.Ecclésiaste 10.8 Psaumes 7.15-7.16 Proverbes 5.22 1 Rois 2.44 1 Samuel 12.3-12.4
7 Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia.Proverbes 10.28 Job 8.13-8.14 Job 11.20 Psaumes 146.4 Proverbes 14.32
8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake.Proverbes 21.18 Esther 7.9-7.10 Esaïe 43.3-43.4 Daniel 6.23-6.24
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.1 Rois 22.20-22.23 1 Rois 13.18-13.22 Psaumes 55.12 Proverbes 2.10-2.16 Marc 13.14
10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.Proverbes 28.12 Job 27.23 Esther 8.15-8.16 Psaumes 58.10-58.11 Proverbes 28.28
11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.Proverbes 29.8 Proverbes 14.34 Job 22.30 2 Samuel 20.1 Genèse 45.8
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.Proverbes 14.21 Néhémie 4.2-4.4 2 Rois 18.36 Luc 16.14 Proverbes 10.19
13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.Proverbes 20.19 Lévitique 19.16 Jérémie 38.27 Josué 2.14 1 Timothée 5.13
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.Proverbes 15.22 Proverbes 24.6 Proverbes 20.18 1 Rois 12.1-12.19 Esaïe 19.11-19.14
15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.Proverbes 17.18 Proverbes 20.16 Proverbes 6.1-6.5 Proverbes 22.26-22.27
16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote.Proverbes 31.30-31.31 1 Samuel 25.32-25.33 Luc 10.42 Matthieu 26.13 2 Samuel 20.16-20.22
17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.Matthieu 5.7 Matthieu 25.34-25.40 Philippiens 4.17 Ecclésiaste 4.8 Jacques 5.1-5.5
18 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika.Osée 10.12-10.13 Jacques 3.18 Galates 6.8-6.9 Ecclésiaste 10.8 Proverbes 22.8
19 Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.Proverbes 10.16 Proverbes 19.23 Proverbes 12.28 Romains 6.23 Proverbes 1.16-1.19
20 Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa Bwana; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.1 Chroniques 29.17 Psaumes 119.1 Proverbes 16.17 Psaumes 18.25-18.26 Proverbes 15.8
21 Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka.Proverbes 16.5 Actes 2.39 Jérémie 32.39 Psaumes 112.1-112.2 Proverbes 13.22
22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.Proverbes 31.30 Nahum 3.4-3.6 Ezéchiel 16.15-16.22 Proverbes 7.10 1 Pierre 3.3-3.4
23 Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.Romains 2.8-2.9 Proverbes 10.28 Hébreux 10.27 Psaumes 37.4 Psaumes 27.4
24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.Proverbes 19.17 Psaumes 112.9 Luc 6.38 2 Corinthiens 9.5-9.11 Deutéronome 15.10
25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.2 Corinthiens 9.6-9.9 Matthieu 5.7 Esaïe 32.8 Proverbes 28.27 Esaïe 58.7-58.11
26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.Job 29.13 Genèse 42.6 Proverbes 24.24 Amos 8.4-8.6
27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia.Psaumes 7.15-7.16 Esther 7.10 Psaumes 57.6 Psaumes 9.15-9.16 Proverbes 17.11
28 Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani.Jérémie 17.8 1 Timothée 6.17 Psaumes 1.3 Psaumes 49.6 Job 31.24-31.25
29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.Ecclésiaste 5.16 Proverbes 14.19 1 Samuel 25.17 Habakuk 2.9-2.10 Proverbes 15.27
30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu.Daniel 12.3 Jacques 5.20 Proverbes 3.18 1 Corinthiens 9.19-9.23 1 Thessaloniciens 2.19
31 Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?Jérémie 25.29 Proverbes 13.21 1 Corinthiens 11.30-11.32 2 Samuel 12.9-12.12 1 Pierre 4.17-4.18

Cette Bible est dans le domaine public.