Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 11
Bible en Swahili de l’est


1 Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Proverbes 16.11 Proverbes 20.23 Proverbes 20.10 Deutéronome 25.13-25.16 Lévitique 19.35-19.36
2 Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Luc 18.14 Proverbes 16.18-16.19 Luc 14.8-14.11 Proverbes 15.33 Proverbes 29.23
3 Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Proverbes 13.6 Psaumes 25.21 Esaïe 1.28 Ecclésiaste 7.17 Jean 7.17
4 Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Genèse 7.1 Sophonie 1.18 Proverbes 10.2 Ezéchiel 7.19 Proverbes 12.28
5 Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Proverbes 5.22 Proverbes 3.6 2 Samuel 17.23 Proverbes 11.3 Esther 7.3-7.10
6 Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Ecclésiaste 10.8 Proverbes 5.22 1 Rois 2.44 Psaumes 7.15-7.16 1 Samuel 12.3-12.4
7 Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Proverbes 10.28 Job 8.13-8.14 Job 11.20 Psaumes 146.4 Proverbes 14.32
8 Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Proverbes 21.18 Esaïe 43.3-43.4 Daniel 6.23-6.24 Esther 7.9-7.10
9 Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. 1 Rois 13.18-13.22 Psaumes 55.12 Proverbes 2.10-2.16 1 Rois 22.20-22.23 2 Thessaloniciens 2.8-2.10
10 Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. Proverbes 28.12 Esther 8.15-8.16 Psaumes 58.10-58.11 Proverbes 28.28 Juges 5.31
11 Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Proverbes 29.8 Proverbes 14.34 2 Samuel 20.1 Genèse 45.8 Jacques 3.6
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Proverbes 14.21 2 Rois 18.36 Luc 16.14 Proverbes 10.19 Juges 9.38
13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Proverbes 20.19 Lévitique 19.16 Josué 2.14 1 Timothée 5.13 Jérémie 38.27
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Proverbes 15.22 Proverbes 24.6 Proverbes 20.18 Esaïe 19.11-19.14 Actes 15.6-15.21
15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama. Proverbes 17.18 Proverbes 6.1-6.5 Proverbes 22.26-22.27 Proverbes 20.16
16 Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. 1 Samuel 25.32-25.33 Proverbes 31.30-31.31 2 Samuel 20.16-20.22 Romains 16.2-16.4 Luc 21.2-21.4
17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Matthieu 5.7 Matthieu 25.34-25.40 Job 20.19-20.23 2 Corinthiens 9.6-9.14 Esaïe 57.1
18 Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. Osée 10.12-10.13 Jacques 3.18 Ecclésiaste 10.8 Galates 6.8-6.9 Proverbes 22.8
19 Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. Proverbes 10.16 Proverbes 19.23 Proverbes 12.28 Proverbes 1.16-1.19 1 Jean 3.10
20 Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa Bwana; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. 1 Chroniques 29.17 Psaumes 119.1 Psaumes 11.7 Psaumes 51.6 Proverbes 8.13
21 Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. Proverbes 16.5 Actes 2.39 Jérémie 32.39 Psaumes 112.1-112.2 Psaumes 37.26
22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili. Proverbes 31.30 Ezéchiel 16.15-16.22 Proverbes 7.10 1 Pierre 3.3-3.4 Genèse 24.47
23 Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Romains 2.8-2.9 Proverbes 10.28 Psaumes 27.4 Psaumes 119.5 Psaumes 119.10
24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Proverbes 19.17 Luc 6.38 2 Corinthiens 9.5-9.11 Psaumes 112.9 Aggée 2.16-2.19
25 Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. 2 Corinthiens 9.6-9.9 Matthieu 5.7 Esaïe 32.8 Proverbes 28.27 Esaïe 58.7-58.11
26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Job 29.13 Genèse 42.6 Proverbes 24.24 Amos 8.4-8.6
27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Psaumes 7.15-7.16 Esther 7.10 Psaumes 57.6 Proverbes 17.11 Psaumes 9.15-9.16
28 Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Jérémie 17.8 1 Timothée 6.17 Psaumes 1.3 Psaumes 49.6 Job 31.24-31.25
29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Ecclésiaste 5.16 Proverbes 14.19 Habakuk 2.9-2.10 Proverbes 15.27 Josué 7.24-7.25
30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. Daniel 12.3 Jacques 5.20 Proverbes 3.18 1 Corinthiens 9.19-9.23 1 Thessaloniciens 2.19
31 Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi? Jérémie 25.29 1 Corinthiens 11.30-11.32 2 Samuel 12.9-12.12 1 Pierre 4.17-4.18 2 Samuel 7.14-7.15

Cette Bible est dans le domaine public.