Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 15.5
Bible en Swahili de l’est


1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.Proverbes 25.15 Proverbes 29.22 Proverbes 15.18 1 Samuel 25.21-25.33 1 Rois 12.13-12.16
2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.Proverbes 12.23 Proverbes 15.28 Proverbes 13.16 Esaïe 50.4 Psaumes 59.7
3 Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.Hébreux 4.13 Jérémie 16.17 2 Chroniques 16.9 Jérémie 23.24 Job 31.4
4 Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.Proverbes 3.18 Proverbes 16.24 Proverbes 12.18 Proverbes 18.14 1 Timothée 6.3
5 Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara.Proverbes 13.1 Proverbes 15.31-15.32 Proverbes 13.18 Proverbes 10.1 2 Samuel 15.1-15.6
6 Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu.Proverbes 8.21 Proverbes 21.20 Proverbes 10.22 Psaumes 112.3 Job 20.19-20.23
7 Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.Matthieu 12.34 Psaumes 45.2 Marc 16.15 Psaumes 71.15-71.18 Psaumes 78.2-78.6
8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.Proverbes 15.29 1 Chroniques 29.17 Jérémie 6.20 Proverbes 21.27 Esaïe 61.8
9 Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.1 Timothée 6.11 Proverbes 21.21 Psaumes 1.6 Proverbes 21.8 Jérémie 44.4
10 Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa.Proverbes 5.12 Proverbes 12.1 1 Rois 21.20 Ezéchiel 24.13-24.14 1 Rois 18.17
11 Kuzimu na Uharibifu vi wazi mbele za Bwana; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?Psaumes 44.21 2 Chroniques 6.30 Job 26.6 Psaumes 139.8 Hébreux 4.13
12 Mwenye mzaha hapendi kukaripiwa; Wala yeye hawaendei wenye hekima.Amos 5.10 Proverbes 9.7-9.8 2 Chroniques 18.7 2 Timothée 4.3 Proverbes 15.10
13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.Proverbes 17.22 Proverbes 12.25 Proverbes 18.14 Proverbes 15.15 2 Corinthiens 1.12
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.Proverbes 9.9 1 Rois 3.6-3.12 Esaïe 44.20 Proverbes 1.5 Actes 17.11
15 Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima.Proverbes 17.22 Proverbes 15.13 2 Corinthiens 6.10 Romains 12.12 Romains 5.11
16 Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.1 Timothée 6.6 Proverbes 16.8 Psaumes 37.16 Ecclésiaste 5.10-5.12 Proverbes 10.22
17 Chakula cha mboga penye mapendano; Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.Proverbes 17.1 Proverbes 21.19 Matthieu 22.4 1 Jean 4.16 Psaumes 133.1-133.3
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.Proverbes 26.21 Proverbes 29.22 Proverbes 14.29 Proverbes 28.25 Ecclésiaste 10.4
19 Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.Proverbes 22.5 Proverbes 26.13 Proverbes 22.13 Proverbes 8.9 Nombres 14.7-14.9
20 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye.Proverbes 10.1 Proverbes 29.3 Proverbes 30.17 1 Rois 1.48 Lévitique 19.3
21 Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.Ephésiens 5.15 Proverbes 10.23 Jacques 3.13 Proverbes 11.12 Job 28.28
22 Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.Proverbes 11.14 Proverbes 20.18 Ecclésiaste 8.6
23 Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!Esaïe 50.4 Proverbes 12.14 Proverbes 16.13 Proverbes 25.11-25.12 Ephésiens 4.29
24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.Philippiens 3.20 Proverbes 2.18 Colossiens 3.1-3.2 Proverbes 7.27 Matthieu 7.14
25 Bwana ataing’oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.Psaumes 146.9 Proverbes 23.10 Proverbes 12.7 Psaumes 68.5-68.6 Proverbes 14.11
26 Mashauri mabaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maneno yapendezayo ni safi.Jérémie 4.14 Psaumes 19.14 Matthieu 12.34-12.37 Proverbes 24.9 Proverbes 15.23
27 Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.Exode 23.8 Jérémie 17.11 2 Rois 5.27 Deutéronome 16.19 Proverbes 11.29
28 Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.1 Pierre 3.15 Proverbes 15.2 1 Rois 3.23-3.28 Proverbes 10.19 Proverbes 13.16
29 Bwana yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.Jean 9.31 Proverbes 15.8 Psaumes 145.18-145.19 1 Pierre 3.12 Psaumes 66.18-66.19
30 Mng’ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.Proverbes 25.25 Ecclésiaste 11.7 Apocalypse 22.5 Proverbes 13.9 Proverbes 17.22
31 Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai Litakaa kati yao wenye hekima.Proverbes 15.5 Proverbes 25.12 Proverbes 19.20 1 Jean 2.19 Proverbes 13.20
32 Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.Proverbes 1.24-1.33 Jacques 1.22 Apocalypse 3.19 Proverbes 1.7 Matthieu 7.24-7.27
33 Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.Proverbes 18.12 Proverbes 1.7 1 Pierre 5.5 Jacques 4.10 Proverbes 29.23

Cette Bible est dans le domaine public.