Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 31
Bible en Swahili de l’est


1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Proverbes 6.20 2 Timothée 1.5 2 Timothée 3.15 Proverbes 1.8 Proverbes 30.1
2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? Esaïe 49.15 1 Samuel 1.11 1 Samuel 1.28
3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme. Néhémie 13.26 Deutéronome 17.17 Proverbes 5.9-5.11 1 Rois 11.1 Proverbes 7.26-7.27
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? Ecclésiaste 10.17 Proverbes 20.1 Esaïe 5.22 Habakuk 2.5 Lévitique 10.9-10.10
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. Habakuk 2.5
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. 1 Timothée 5.23 1 Samuel 30.6 Job 3.20 Psaumes 104.15 2 Rois 4.27
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake. Ephésiens 5.18
8 Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Psaumes 82.3-82.4 Proverbes 24.11-24.12 Jérémie 26.16-26.19 Jérémie 26.24 Jean 7.51
9 Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao. Esaïe 1.17 Deutéronome 1.16 Lévitique 19.15 Job 29.15-29.16 Jérémie 22.15-22.16
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Proverbes 19.14 Proverbes 12.4 Proverbes 18.22 Ruth 3.11 Ephésiens 5.25-5.33
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. 2 Rois 4.9-4.10 1 Pierre 3.1-3.7 2 Rois 4.22-4.23
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. 1 Samuel 25.26-25.27 1 Samuel 25.18-25.22
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. 1 Timothée 5.10 Genèse 24.13-24.14 Ruth 2.23 Esaïe 32.9-32.11 Esaïe 3.16-3.24
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. 1 Rois 9.26-9.28 Proverbes 31.24 Ezéchiel 27.3-27.36 2 Chroniques 9.10
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Luc 12.42 Romains 12.11 Marc 1.35 Proverbes 20.13 Ecclésiaste 9.10
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Matthieu 13.44 Josué 15.18 Cantique 8.12
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. 1 Rois 18.46 Job 38.3 2 Rois 4.29 1 Pierre 1.13 Ephésiens 6.10
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Psaumes 127.2 2 Thessaloniciens 3.7-3.9 Genèse 31.40 1 Thessaloniciens 2.9 Matthieu 25.3-25.10
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Exode 35.25-35.26
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Ephésiens 4.28 Proverbes 22.9 Hébreux 13.16 Job 31.16-31.20 Romains 10.21
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Proverbes 25.20 Genèse 45.22 2 Samuel 1.24
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Proverbes 7.16 Genèse 41.42 Apocalypse 19.14 Psaumes 45.13-45.14 Esther 5.1
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Ruth 4.1 Proverbes 12.4 Deutéronome 16.18 Ruth 4.11 Deutéronome 21.19
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Ezéchiel 27.16 Proverbes 31.19 1 Rois 10.28 Proverbes 31.13 Luc 16.19
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Psaumes 132.16 Esaïe 65.13-65.14 Esaïe 61.10 Job 29.14 Ephésiens 4.24
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake. Proverbes 10.31 Ephésiens 4.29 Luc 1.42-1.56 1 Pierre 3.4-3.5 Esther 7.3-7.6
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Proverbes 14.1 Tite 2.4 1 Timothée 5.10 1 Thessaloniciens 4.11 2 Thessaloniciens 3.6
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, 2 Timothée 3.15-3.17 Proverbes 31.1 1 Rois 2.19 Esaïe 62.4-62.5 Psaumes 116.16
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Cantique 6.8-6.9 Ephésiens 5.27
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa. 1 Pierre 3.4-3.5 Proverbes 11.22 Proverbes 6.25 Psaumes 147.11 Luc 1.6
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni. Matthieu 7.20 Romains 6.21-6.22 Hébreux 6.10 Romains 16.12 Proverbes 11.30

Cette Bible est dans le domaine public.