Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 31.7
Bible en Swahili de l’est


1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.Proverbes 6.20 2 Timothée 1.5 2 Timothée 3.15 Proverbes 1.8 Proverbes 30.1
2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?Esaïe 49.15 1 Samuel 1.11 1 Samuel 1.28
3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.Néhémie 13.26 Deutéronome 17.17 Proverbes 5.9-5.11 Osée 4.11 1 Rois 11.1
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?Ecclésiaste 10.17 Proverbes 20.1 Esaïe 5.22 Osée 4.11-4.12 Esaïe 28.7-28.8
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.Habakuk 2.5
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.1 Timothée 5.23 1 Samuel 1.10 Job 29.13 1 Samuel 30.6 Job 3.20
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.Ephésiens 5.18
8 Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;Psaumes 82.3-82.4 1 Samuel 22.14-22.15 Jérémie 38.7-38.10 Proverbes 24.11-24.12 Jérémie 26.16-26.19
9 Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.Esaïe 1.17 Lévitique 19.15 Deutéronome 1.16 Job 29.15-29.16 Jérémie 22.15-22.16
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.Proverbes 19.14 Proverbes 12.4 Proverbes 18.22 Ruth 3.11 Ephésiens 5.25-5.33
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.2 Rois 4.9-4.10 1 Pierre 3.1-3.7 2 Rois 4.22-4.23
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.1 Samuel 25.26-25.27 1 Samuel 25.18-25.22
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.1 Timothée 5.10 Tite 2.5 Actes 9.39-9.40 1 Thessaloniciens 4.11 Genèse 29.9-29.10
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.1 Rois 9.26-9.28 Proverbes 31.24 Ezéchiel 27.3-27.36 2 Chroniques 9.10
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.Luc 12.42 Romains 12.11 2 Chroniques 36.15 Psaumes 119.147-119.148 Josué 3.1
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.Matthieu 13.44 Josué 15.18 Cantique 8.12
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.1 Pierre 1.13 1 Rois 18.46 Job 38.3 2 Rois 4.29 Ephésiens 6.14
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.Psaumes 127.2 2 Thessaloniciens 3.7-3.9 Genèse 31.40 1 Thessaloniciens 2.9 Matthieu 25.3-25.10
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.Exode 35.25-35.26
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.Ephésiens 4.28 Proverbes 22.9 Hébreux 13.16 Job 31.16-31.20 Psaumes 112.9
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.Proverbes 25.20 Genèse 45.22 2 Samuel 1.24
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.Genèse 41.42 Proverbes 7.16 Apocalypse 19.14 1 Pierre 3.3 Juges 8.26
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.Ruth 4.1 Deutéronome 16.18 Proverbes 12.4 Proverbes 24.7 Ruth 4.11
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.Ezéchiel 27.16 Juges 14.12 Proverbes 31.19 1 Rois 10.28 Proverbes 31.13
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.Psaumes 97.11-97.12 Psaumes 132.9 Job 40.10 Psaumes 132.16 Esaïe 65.13-65.14
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.Proverbes 10.31 Ephésiens 4.29 Proverbes 31.8-31.9 2 Samuel 20.16-20.22 Proverbes 25.15
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.Proverbes 14.1 Tite 2.4 1 Timothée 5.10 1 Thessaloniciens 4.11 2 Thessaloniciens 3.6
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,2 Timothée 3.15-3.17 Cantique 7.1-7.9 Proverbes 31.1 1 Rois 2.19 Esaïe 62.4-62.5
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.Cantique 6.8-6.9 Ephésiens 5.27
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.1 Pierre 3.4-3.5 Proverbes 11.22 Proverbes 6.25 2 Samuel 14.25 Psaumes 147.11
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.Apocalypse 14.13 1 Timothée 5.25 Marc 14.7-14.9 Philippiens 4.17 Matthieu 7.16

Cette Bible est dans le domaine public.