Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 27
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Jérémie 27.3 Jérémie 26.1 2 Chroniques 36.11 Jérémie 28.1 Jérémie 27.12
2 Bwana ameniambia hivi, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike shingoni; Amos 7.4 Jérémie 28.10-28.14 Jérémie 27.12 Esaïe 20.2-20.4 Ezéchiel 12.1-12.28
3 kisha uvipeleke kwa mfalme wa Edomu, na mfalme wa Moabu, na mfalme wa wana wa Amoni, na mfalme wa Tiro, na mfalme wa Sidoni, kwa mikono ya wajumbe watakaofika Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda. Amos 1.9-2.3 Ezéchiel 29.18 Ezéchiel 25.1-25.17 Ezéchiel 17.15-17.21 Jérémie 25.19-25.26
4 Uwaagize waende kwa bwana zao, na kuwaambia, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Mtawaambia bwana zenu maneno haya; Jérémie 10.10 Jérémie 51.19 Exode 5.1 Jérémie 10.16 Jérémie 25.27
5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo. Esaïe 42.5 Jérémie 32.17 Esaïe 45.12 Psaumes 146.5-146.6 Psaumes 115.15-115.16
6 Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama wa mwituni pia nimempa wamtumikie. Jérémie 28.14 Jérémie 25.9 Ezéchiel 29.18-29.20 Esaïe 44.28 Jérémie 43.10
7 Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye. Jérémie 52.31 Zacharie 2.8-2.9 Esaïe 14.4-14.6 Jérémie 50.1-50.46 Apocalypse 18.2-18.8
8 Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadreza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema Bwana, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake. Jérémie 38.17-38.19 Jérémie 24.10 Ezéchiel 17.19-17.21 Ezéchiel 14.21 Jérémie 40.9
9 Lakini, katika habari zenu, msisikilize manabii wenu, wala wabashiri wenu, wala ndoto zenu, wala watambuzi wenu, wala waganga wenu, wanaowaambia, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli; Esaïe 8.19 Malachie 3.5 Jérémie 29.8 Jérémie 14.14 Jérémie 27.14-27.16
10 maana wanawatabiria uongo, ili kuwatoa ninyi mbali na nchi yenu; niwafukuze mkaangamie. Jérémie 32.31 Jérémie 28.16 Ezéchiel 14.9-14.11 Jérémie 27.14 Lamentations 2.14
11 Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema Bwana; nao watailima, na kukaa ndani yake. Jérémie 27.2 Jérémie 27.8 Jérémie 21.9 Jérémie 27.12 Jérémie 38.2
12 Nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa mfano wa maneno hayo yote, nikisema, Tieni shingo zenu katika nira ya mfalme wa Babeli, mkamtumikie yeye na watu wake, mpate kuishi. Jérémie 38.17 Jérémie 28.1 Proverbes 1.33 Jérémie 27.2-27.3 Jérémie 27.8
13 Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama Bwana alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli? Ezéchiel 18.31 Jérémie 27.8 Proverbes 8.36 Ezéchiel 33.11 Ezéchiel 14.21
14 Wala msisikilize maneno ya manabii wawaambiao ninyi, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli; maana wanawatabiria uongo. Jérémie 14.14 Jérémie 29.8-29.9 Jérémie 27.9-27.10 2 Corinthiens 11.13-11.15 Jérémie 23.21
15 Kwa maana mimi sikuwatuma, asema Bwana, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria. Jérémie 27.10 Jérémie 6.13-6.15 2 Chroniques 25.16 Jérémie 14.15-14.16 Jérémie 8.10-8.12
16 Pia nalisema na makuhani, na watu wote, nikisema, Bwana asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya Bwana, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo. Jérémie 28.3 2 Rois 24.13 Jérémie 27.10 Daniel 1.2 Jérémie 27.14
17 Msiwasikilize; mtumikieni mfalme wa Babeli, mkaishi; kwani mji huu kufanywa ukiwa? Jérémie 38.17 Jérémie 27.11-27.13 Jérémie 38.23 Jérémie 7.34
18 Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la Bwana liko kwao, basi na wamwombe Bwana wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya Bwana, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli. 1 Samuel 7.8 1 Rois 18.24 1 Samuel 12.19 Jérémie 18.20 1 Samuel 12.23
19 Maana Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari za nguzo, na katika habari za bahari, na katika habari za matako yake, na katika habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu, 2 Rois 25.13 Jérémie 52.17-52.23 2 Rois 25.17 1 Rois 7.15-7.22 2 Chroniques 4.2-4.16
20 ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu; Jérémie 24.1 2 Chroniques 36.10 2 Rois 24.14-24.16 2 Chroniques 36.18 Jérémie 22.28
21 naam, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Bwana, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu; 22 Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijilia, asema Bwana; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa. Jérémie 29.10 Esdras 7.19 Jérémie 32.5 Esdras 1.11 Esdras 5.13-5.15

Cette Bible est dans le domaine public.