11 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; Nombres 10.10 Ezéchiel 46.6 Colossiens 2.16 2 Chroniques 2.4 1 Samuel 20.5 12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; Nombres 15.4-15.12 Nombres 29.10 Ezéchiel 46.5-46.7 13 na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 14 Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng’ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15 Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. Nombres 28.3 Nombres 28.22 Nombres 15.24 Lévitique 4.23 Lévitique 16.15
Les sacrifices de la Pâque
16 Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya Bwana. Exode 12.18 Exode 12.2-12.11 Deutéronome 16.1-16.8 Lévitique 23.5-23.8 Actes 12.3-12.4 17 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba. Lévitique 23.6 Exode 34.18 Exode 12.15-12.17 Deutéronome 16.3-16.8 Exode 23.15 18 Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; Exode 12.16 Lévitique 23.7-23.8 19 lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana; ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; Deutéronome 15.21 Nombres 29.8 Nombres 28.31 Lévitique 22.20 Ezéchiel 45.21-45.25 20 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume; 21 na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba; 22 tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Romains 8.3 23 Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. Nombres 28.3 Nombres 28.10 24 Mtasongeza sadaka kwa mfano huu kila siku muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 25 Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi. Lévitique 23.8 Exode 12.16 Nombres 28.18 Exode 13.6 Lévitique 23.35-23.36
Les sacrifices de la fête des moissons
26 Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsongezea Bwana sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; Exode 23.16 Exode 34.22 Lévitique 23.10 Lévitique 23.15-23.21 Deutéronome 16.9-16.11 27 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe waume wadogo wawili, kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; Lévitique 23.18-23.19 Nombres 28.11 Nombres 28.19 28 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, 29 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba; 30 na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Nombres 28.22 Nombres 28.15 1 Pierre 3.18 Nombres 15.24 Galates 3.13 31 Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji. Nombres 28.19 Nombres 28.3 Malachie 1.13-1.14