Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Deutéronome 10.13
Bible en Swahili de l’est


1 Wakati ule Bwana akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti.Exode 34.1-34.2 Hébreux 9.4 Deutéronome 10.3-10.4 Exode 25.10-25.15 Exode 34.4
2 Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku.Exode 25.16-25.22 Hébreux 9.4 Exode 40.20 1 Rois 8.9 Deutéronome 4.13
3 Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu.Exode 34.4 Exode 37.1-37.9 Exode 25.10 Exode 25.5 Deutéronome 10.1
4 Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia Bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; Bwana akanipa.Deutéronome 9.10 Exode 34.28 Deutéronome 18.16 Exode 19.17-19.18 Deutéronome 5.4-5.26
5 Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru Bwana.Exode 40.20 Exode 34.29 Deutéronome 9.15 Josué 4.9 1 Rois 8.8-8.9
6 (Wana wa Israeli wakasafiri kutoka visima vya Bene-Yaakani kwenda Mosera; Haruni akafa huko, akazikwa huko; na Eleazari mwanawe alitumika utumishi wa ukuhani badala yake.Nombres 33.38 Nombres 20.23-20.28 Nombres 33.30-33.33 Nombres 10.12-10.13 Nombres 33.1-33.2
7 Wakasafiri kutoka huko kwenda Gudgoda; wakatoka Gudgoda wakaenda Yotbatha, nayo ni nchi ya vijito vya maji.Nombres 33.32-33.34
8 Na wakati huo Bwana aliitenga kabila ya Lawi ili walichukue lile sanduku la agano la Bwana, wasimame mbele ya Bwana kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.Deutéronome 18.5 Deutéronome 21.5 2 Chroniques 30.27 Nombres 6.23-6.26 Lévitique 9.22
9 Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; Bwana ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia Bwana, Mungu wako.)Deutéronome 18.1-18.2 Ezéchiel 44.28 Josué 14.3 Nombres 18.20-18.24 Nombres 26.62
10 Nikakaa mle mlimani kama hapo kwanza, siku arobaini usiku na mchana; Bwana akanisikiza wakati huo nao; asitake Bwana kukuangamiza.Deutéronome 9.18-9.19 Deutéronome 9.25 Exode 34.28 Exode 33.17 Exode 32.14
11 Bwana akaniambia, Ondoka, ushike safari yako mbele ya watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa.Exode 32.34 Exode 33.1
12 Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;Deutéronome 6.5 Michée 6.8 Deutéronome 5.33 Luc 10.27 Deutéronome 11.13
13 kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?Deutéronome 6.24 Jacques 1.25 Proverbes 9.12 Jérémie 32.39
14 Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.1 Rois 8.27 Néhémie 9.6 Exode 19.5 Psaumes 24.1 Psaumes 115.16
15 Tena, Bwana aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo.Deutéronome 4.37 Nombres 14.8 Romains 9.13-9.23 Deutéronome 7.7-7.8
16 Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu.Jérémie 4.4 Deutéronome 30.6 Lévitique 26.41 Deutéronome 9.6 Romains 2.28-2.29
17 Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.Galates 2.6 Apocalypse 17.14 Apocalypse 19.16 Josué 22.22 Ephésiens 6.9
18 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.Psaumes 146.9 Psaumes 68.5 Matthieu 5.45 Jérémie 49.11 Actes 14.17
19 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.Exode 22.21 Lévitique 19.33-19.34 Jacques 2.15-2.16 Luc 6.35 Luc 10.28-10.37
20 Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.Deutéronome 13.4 Deutéronome 6.13 Matthieu 4.10 Deutéronome 11.22 Luc 4.8
21 Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.Jérémie 17.14 Psaumes 106.21-106.22 2 Samuel 7.23 Exode 15.2 Psaumes 22.3
22 Baba zako walishukia Misri na watu sabini; na sasa Bwana, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.Genèse 15.5 Genèse 46.27 Exode 1.5 Deutéronome 1.10 Actes 7.14

Cette Bible est dans le domaine public.