22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. Psaumes 107.13-107.14 Lévitique 26.44 Psaumes 106.44-106.45 Deutéronome 32.36 23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. 1 Samuel 5.2-5.5 Michée 4.5 1 Corinthiens 10.20 Romains 1.23-1.25 Job 30.9-30.10 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. Daniel 5.4 Esaïe 37.20 Habakuk 1.16 Juges 15.16 1 Samuel 31.9 25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. 2 Samuel 13.28 Juges 9.27 Juges 19.6 Matthieu 27.29 Daniel 5.2-5.3 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea. 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Deutéronome 22.8 Josué 2.8 2 Samuel 11.2 Juges 9.51 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili. Jérémie 15.15 Psaumes 74.18-74.23 Psaumes 91.15 2 Chroniques 20.12 Juges 15.18 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. 30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake. Matthieu 16.25 Job 20.5 1 Thessaloniciens 5.2 Juges 14.19 Juges 15.8 31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini. Juges 15.20 Juges 13.2 Juges 13.25 Josué 19.41 Jean 19.39-19.42