22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. Psaumes 106.44-106.45 Deutéronome 32.36 Psaumes 107.13-107.14 Lévitique 26.44 23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. 1 Samuel 5.2-5.5 Romains 1.23-1.25 Job 30.9-30.10 1 Corinthiens 8.4-8.5 Proverbes 24.17 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. Daniel 5.4 Juges 15.16 1 Samuel 31.9 Juges 15.8 Ezéchiel 20.14 25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. Juges 19.6 2 Samuel 13.28 Juges 9.27 Matthieu 27.39-27.44 Esther 3.15 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea. 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Deutéronome 22.8 2 Samuel 11.2 Josué 2.8 Juges 9.51 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili. Jérémie 15.15 Psaumes 74.18-74.23 Psaumes 116.4 Juges 5.31 Hébreux 11.32 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. 30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake. Matthieu 16.25 Actes 21.13 Job 31.3 Psaumes 62.3 Genèse 3.15 31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini. Juges 15.20 Juges 13.25 Juges 13.2 Jean 19.39-19.42 Josué 19.41