Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 50.7
Bible en Swahili de l’est


1 Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu.Genèse 46.4 1 Thessaloniciens 4.13 Marc 5.38-5.39 Jean 11.35-11.38 Ephésiens 6.4
2 Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga, kwamba wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli.2 Chroniques 16.14 Genèse 50.26 Marc 16.1 Jean 19.39-19.40 Matthieu 26.12
3 Siku zake arobaini zikaisha, maana hivyo hutimizwa siku za kupaka dawa. Wamisri wakamlilia siku sabini.Deutéronome 34.8 Nombres 20.29 Genèse 50.10 Deutéronome 21.13
4 Siku za kumlilia zilipopita, Yusufu alisema na watu wa nyumba ya Farao, akinena, Kama nimeona neema machoni penu, tafadhalini mkaseme masikioni mwa Farao, mkinena, Baba yangu aliniapisha, akisema,Esther 4.2 Genèse 18.3
5 Mimi ni katika kufa, unizike katika kaburi langu nililojichimbia katika nchi ya Kanaani. Basi tafadhali uniruhusu niende sasa nikamzike babangu, nami nitarudi.Esaïe 22.16 2 Chroniques 16.14 Matthieu 27.60 Genèse 47.29-47.31 1 Samuel 14.43
6 Farao akasema, Uende, ukamzike baba yako, kama alivyokuapisha.Genèse 48.21
7 Basi Yusufu akaenda amzike babaye, na watumwa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, wazee wa nyumbani mwake, na wazee wote wa nchi ya Misri.Genèse 14.16
8 Na nyumba yote ya Yusufu, na nduguze, na nyumba ya babaye; wakawaacha watoto wao tu, na kondoo zao, na ng’ombe zao, katika nchi ya Gosheni.Exode 10.26 Nombres 32.24-32.27 Exode 10.8-10.9
9 Kisha wakaenda pamoja naye wapanda farasi, na magari; wakawa jeshi kubwa sana.Actes 8.2 Exode 14.7 Exode 14.28 Cantique 1.9 2 Rois 18.24
10 Wakaja mpaka sakafu ya Atadi, iliyo ng’ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya babaye siku saba.Actes 8.2 2 Samuel 1.17 Job 2.13 1 Samuel 31.13 Deutéronome 1.1
11 Nao waliokaa katika nchi, wale Wakanaani, walipoyaona matanga katika sakafu ya Atadi, wakasema, Matanga haya ya Wamisri ni makuu kwa hiyo mahali pale paliitwa Abel-Misri, iliyo ng’ambo ya Yordani.Deutéronome 11.30 Deutéronome 3.25 Genèse 34.30 Genèse 50.10 Genèse 24.6
12 Wanawe wakamfanyia kama alivyo waagiza;Exode 20.12 Genèse 47.29-47.31 Actes 7.16 Genèse 49.29-49.32 Ephésiens 6.1
13 kwa kuwa wanawe wakamchukuwa mpaka nchi ya Kanaani, nao wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia.Actes 7.16 Genèse 49.29-49.31 Genèse 23.16-23.18 Genèse 35.27 Genèse 23.20
14 Yusufu akarudi Misri, yeye na ndugu zake, na wote waliyokwenda pamoja naye kumzika babaye, baada ya kumzika babaye. 15 Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.Proverbes 28.1 Psaumes 53.5 Psaumes 14.5 Lévitique 26.36 Genèse 42.21-42.22
16 Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema,Proverbes 29.25
17 Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.Psaumes 21.11 Proverbes 28.13 Genèse 45.8 Genèse 50.20 Matthieu 6.14-6.15
18 Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako.Genèse 37.7-37.11 Genèse 27.29 Genèse 44.14 Genèse 42.6 Genèse 45.3
19 Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu?Romains 12.19 Genèse 30.2 2 Rois 5.7 Job 34.19-34.29 Genèse 45.5
20 Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.Romains 8.28 Psaumes 119.71 Genèse 45.5-45.8 Actes 3.26 Genèse 37.4
21 Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.Genèse 47.12 1 Pierre 3.9 Matthieu 5.44 Matthieu 6.14 Esaïe 40.2
22 Akakaa Yusufu katika Misri, yeye na nyumba ya babaye. Akaishi Yusufu miaka mia na kumi. 23 Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu.Job 42.16 Nombres 32.39 Genèse 30.3 Psaumes 128.6 Josué 17.1
24 Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.Genèse 35.12 Genèse 26.3 Exode 3.16-3.17 Genèse 48.21 Genèse 46.4
25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.Exode 13.19 Josué 24.32 Hébreux 11.22 Actes 7.16 Genèse 47.29-47.31
26 Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.Genèse 47.9 Genèse 47.28 Genèse 50.2-50.3 Genèse 50.22 Josué 24.29

Cette Bible est dans le domaine public.