Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 35.14
Bible en Swahili de l’est


1 Musa akakutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli, na kuwaambia, Maneno aliyoyausia Bwana ni haya, kwamba myafanye.Exode 34.32 Exode 31.1-31.11 Matthieu 7.21-7.27 Jacques 1.22 Exode 25.1-25.40
2 Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa Bwana; mtu awaye yote atakayefanya kazi yo yote katika siku hiyo atauawa.Exode 20.9-20.10 Lévitique 23.3 Exode 34.21 Nombres 15.32-15.36 Exode 23.12
3 Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato.Exode 16.23 Nombres 15.32-15.36 Exode 12.16 Esaïe 58.13
4 Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru Bwana, akisema,Exode 25.1-25.2
5 Katwaeni kati yenu matoleo kwa Bwana; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;Exode 25.2-25.7 Psaumes 110.3 2 Corinthiens 9.7 Marc 12.41-12.44 Juges 5.9
6 na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi;Exode 26.7-26.14 Exode 26.36 Exode 28.33 Exode 28.15 Exode 26.31
7 na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na mbao za mshita; 8 na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri;Exode 30.28 Exode 25.1-25.40 Exode 27.20 Exode 30.23
9 na vito vya shohamu, na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.Exode 28.9 Exode 39.6-39.14 Exode 25.5 Exode 28.17-28.21
10 Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo Bwana ameyaagiza;Exode 31.1-31.6 Exode 36.1-36.4
11 yaani, hiyo maskani na hema yake, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, na mataruma yake, na viguzo vyake, na matako yake;Exode 26.1-26.37 Exode 31.7-31.9 Exode 36.8-36.34
12 hilo sanduku, na miti yake, na hicho kiti cha rehema, na lile pazia la sitara;Exode 25.10-25.22 Exode 26.7 Exode 37.1-37.9 Exode 26.31-26.33 Exode 36.35-36.36
13 na hiyo meza, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na hiyo mikate ya wonyesho;Exode 25.23-25.30 Lévitique 24.5-24.6 Exode 37.10-37.16
14 na hicho kinara cha taa kwa mwanga, na vyombo vyake, na taa zake, na hayo mafuta kwa nuru;Exode 25.31-25.39 Exode 37.17-37.24 Psaumes 148.3 Matthieu 5.14-5.15
15 na hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba, na miti yake, na hayo mafuta ya kupaka, na huo uvumba mzuri, na hicho kisitiri cha mlango, mlangoni mwa hiyo maskani;Exode 30.1-30.10 Exode 26.36-26.37 Psaumes 141.2 Exode 30.22-30.38 Exode 37.25-37.28
16 na hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na wavu wake wa shaba, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na hilo birika na tako lake;Exode 27.1-27.8 Exode 30.18-30.21 Exode 38.1-38.8
17 na hizo kuta za nguo za ua, na viguzo vyake, na matako yake, na pazia la lango la ua;2 Samuel 7.2 Exode 27.9-27.19 Exode 38.9-38.20
18 na vile vigingi vya maskani, na vigingi vya ua, na kamba zakeExode 27.19
19 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, kwa ajili ya kutumika ndani ya mahali patakatifu, hayo mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.Exode 31.10 Exode 39.41 Exode 28.1-28.43 Nombres 4.5-4.15 Exode 39.1-39.31
20 Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. 21 Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa Bwana, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.Exode 25.2 Exode 36.2 Exode 35.22 Exode 35.26 Exode 35.5
22 Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa Bwana.Esaïe 60.13 Esdras 2.68-2.69 Ezéchiel 16.11 Esaïe 60.9 Matthieu 2.11
23 Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi, na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, akavileta.1 Chroniques 29.8 Exode 35.6-35.10 Exode 25.2-25.7
24 Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya Bwana; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yo yote ya huo utumishi, akauleta.2 Corinthiens 8.12
25 Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri.Romains 16.6 Actes 9.39 Romains 16.1-16.4 Exode 31.6 Exode 28.3
26 Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi.Exode 35.21 Exode 36.8 Exode 35.29
27 Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani,1 Chroniques 29.6 Esdras 2.68 Exode 35.9
28 na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri.Exode 30.23-30.38 Exode 35.8
29 Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa Bwana kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo Bwana aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.Exode 35.4 1 Chroniques 29.17 Juges 5.2 1 Chroniques 29.3 Deutéronome 4.2
30 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;Exode 31.1-31.6 Jacques 1.17 1 Corinthiens 3.10 1 Corinthiens 12.11 Esaïe 28.26
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;Esaïe 61.1-61.3 Jacques 1.17 Esaïe 28.26 Esaïe 11.2-11.5 2 Chroniques 2.14
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, 33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina. 34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.Exode 31.6 2 Chroniques 2.14 Esdras 7.10 Esdras 7.27 1 Corinthiens 1.5-1.7
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.Exode 35.31 1 Rois 7.14 Exode 31.6 Esaïe 28.26 Exode 31.3

Cette Bible est dans le domaine public.