Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 25.23
Bible en Swahili de l’est


1 Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili.Proverbes 1.1 1 Rois 4.32 Michée 1.1 Ecclésiaste 12.9 Osée 1.1
2 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.Deutéronome 29.29 1 Rois 3.9-3.28 Job 29.16 Romains 11.33-11.34 Job 11.7-11.8
3 Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki.Psaumes 103.11 Esaïe 7.11 1 Pierre 1.7 Esaïe 55.9 Romains 8.39
4 Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;2 Timothée 2.20-2.21 Proverbes 17.3 Esaïe 1.25-1.27 Ezéchiel 22.18 1 Pierre 1.7
5 Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki.Proverbes 16.12 Proverbes 20.8 Proverbes 29.14 Proverbes 20.28 Psaumes 101.7-101.8
6 Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu;Proverbes 25.27 Proverbes 27.2 Amos 7.12-7.15 Proverbes 16.19 Jérémie 1.6-1.10
7 Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho,Luc 18.14 1 Pierre 5.5 Luc 14.7-14.11 Apocalypse 4.1 Proverbes 16.19
8 Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.Matthieu 5.25 Proverbes 17.14 Proverbes 18.6 Proverbes 14.12 Proverbes 30.33
9 Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine;Proverbes 11.13 Matthieu 18.5-18.17 Proverbes 20.19
10 Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke.Psaumes 119.39
11 Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.Proverbes 15.23 Esaïe 50.4 Ecclésiaste 12.10 Proverbes 24.26
12 Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.Psaumes 141.5 Proverbes 9.8 Proverbes 15.31-15.32 1 Samuel 25.31-25.34 Proverbes 27.5-27.6
13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.Proverbes 13.17 Proverbes 26.6 Philippiens 2.25-2.30 Proverbes 25.25
14 Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.Proverbes 20.6 2 Corinthiens 11.13-11.18 2 Corinthiens 11.31 Luc 14.11 Jude 1.16
15 Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.Proverbes 15.1 Ecclésiaste 10.4 Proverbes 16.14 1 Samuel 25.14 Genèse 32.4-32.21
16 Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika.Proverbes 25.27 Esaïe 7.22 Luc 21.34 Proverbes 23.8 1 Samuel 14.25-14.27
17 Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.Juges 19.18-19.21 Genèse 19.2-19.3
18 Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.Psaumes 57.4 Proverbes 12.18 Jérémie 9.8 Psaumes 140.3 Jérémie 9.3
19 Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.Job 6.14-6.20 2 Chroniques 28.20-28.21 Esaïe 36.6 Esaïe 30.1-30.3 Ezéchiel 29.6-29.7
20 Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.Romains 12.15 Ecclésiaste 3.4 Proverbes 10.26 Job 24.7-24.10 Jacques 5.15
21 Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;Exode 23.4-23.5 Matthieu 5.44 Romains 12.20-12.21 Proverbes 24.17 Luc 10.33-10.36
22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu.2 Samuel 16.12 1 Corinthiens 15.18 Matthieu 10.13
23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.Psaumes 101.5 Psaumes 15.3 Romains 1.30 Proverbes 26.20 2 Corinthiens 12.20
24 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.Proverbes 21.9 Proverbes 19.13 Proverbes 21.19 Proverbes 27.15-27.16
25 Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu, Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.Proverbes 15.30 Psaumes 63.1 1 Timothée 1.15 Apocalypse 22.17 Esaïe 55.1
26 Mwenye haki amwangukiapo mtu mbaya Ni kama chemchemi iliyochafuka, Na kisima kilichokanyagwa.Apocalypse 17.6 Genèse 4.8 1 Samuel 22.14-22.18 2 Chroniques 24.21-24.22 1 Thessaloniciens 2.15
27 Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.Proverbes 27.2 Jean 5.44 Proverbes 25.16 2 Corinthiens 12.11 Philippiens 2.3
28 Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.Proverbes 16.32 2 Chroniques 32.5 1 Samuel 20.30 Néhémie 1.3 Proverbes 22.24

Cette Bible est dans le domaine public.