20 Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu; Esaïe 58.9 Psaumes 145.18 Esaïe 6.5 Daniel 9.16 Esaïe 65.24 21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Luc 1.19 Daniel 8.16 1 Rois 18.36 Daniel 10.16 Hébreux 1.14 22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danielii, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. Daniel 8.16 Zacharie 1.9 Daniel 10.21 Zacharie 6.4-6.5 Apocalypse 4.1 23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya. Matthieu 24.15 Daniel 10.19 Daniel 10.11-10.12 Luc 1.28 Ezéchiel 24.16 24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Jérémie 23.5-23.6 Esaïe 61.1 Esaïe 56.1 Psaumes 45.7 Ezéchiel 4.6 25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Esdras 4.24 Esaïe 9.6 Esaïe 55.4 Jean 1.41 Jean 4.25 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Esaïe 53.8 Nahum 1.8 Marc 13.2 Matthieu 24.2 Marc 9.12 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu. Matthieu 24.15 Esaïe 10.22-10.23 Daniel 12.11 Luc 21.20 Luc 21.24