Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Galates 4.26
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;Galates 4.23 Galates 4.29 2 Rois 11.12 Genèse 24.2-24.3 2 Rois 12.2
2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. 3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.Galates 4.9 Galates 2.4 Colossiens 2.8 Colossiens 2.20 Galates 3.23-3.25
4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,Jean 1.14 Marc 1.15 Ephésiens 1.10 Luc 2.7 Jean 3.16
5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.Ephésiens 1.5 Romains 8.23 Galates 3.26 Jean 1.12 Tite 2.14
6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.Romains 8.15-8.17 Romains 5.5 Romains 8.9 Ephésiens 4.30 Philippiens 1.19
7 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.Galates 3.29-4.2 Galates 4.5-4.6 Romains 8.16-8.17 Galates 3.26 Galates 4.31-5.1
8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.1 Corinthiens 1.21 1 Thessaloniciens 4.5 2 Thessaloniciens 1.8 1 Corinthiens 8.4 Esaïe 37.19
9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?1 Corinthiens 8.3 Romains 8.3 Hébreux 7.18 Galates 3.3 Exode 33.17
10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.Romains 14.5 Colossiens 2.16-2.17 Lévitique 25.13 Lévitique 23.1-23.44 Nombres 28.1-28.29
11 Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha bure kwa ajili yenu.1 Thessaloniciens 3.5 Galates 2.2 1 Corinthiens 15.58 Philippiens 2.16 2 Corinthiens 11.2-11.3
12 Ndugu zangu, nawasihi, iweni kama mimi, maana mimi ni kama ninyi. Hamkunidhulumu kwa lo lote.1 Rois 22.4 2 Corinthiens 2.5 Genèse 34.15 1 Corinthiens 9.20-9.23 Actes 21.21
13 Lakini mwajua ya kuwa naliwahubiri Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili;1 Corinthiens 2.3 2 Corinthiens 12.7-12.10 2 Corinthiens 11.6 Galates 1.6 2 Corinthiens 10.10
14 na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu.Matthieu 10.40 1 Thessaloniciens 2.13 2 Corinthiens 5.20 Malachie 2.7 2 Samuel 19.27
15 Ku wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling’oa macho yenu, mkanipa mimi.Galates 6.4 1 Jean 3.16-3.18 Romains 4.6-4.9 Romains 5.2 Romains 10.2
16 Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?Amos 5.10 Galates 2.5 Jean 7.7 Proverbes 9.8 Psaumes 141.5
17 Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.Romains 16.18 2 Pierre 2.3 2 Corinthiens 11.13-11.15 Matthieu 23.15 Philippiens 2.21
18 Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.Apocalypse 3.19 Philippiens 1.27 Galates 4.13 Philippiens 2.12 Tite 2.14
19 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;Ephésiens 4.13 Romains 8.29 Nombres 11.11-11.12 Jacques 1.18 Philémon 1.10
20 laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.1 Thessaloniciens 2.17-2.18 1 Thessaloniciens 3.9 1 Corinthiens 4.19-4.21
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?Galates 3.23-3.24 Jean 12.34 Matthieu 21.42-21.44 Romains 7.5-7.6 Matthieu 22.29-22.32
22 Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.Genèse 16.15 Genèse 21.10 Genèse 16.2-16.4 Genèse 21.1-21.2
23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.Hébreux 11.11 Genèse 18.10-18.14 Romains 9.7-9.8 Genèse 21.1-21.2 Romains 4.18-4.21
24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.1 Corinthiens 10.11 Genèse 21.9-21.13 Osée 11.10 Galates 3.15-3.21 Deutéronome 33.2
25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.Hébreux 12.18 Psaumes 68.17 Matthieu 23.37 Deutéronome 33.2 Juges 5.5
26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.Hébreux 12.22 Apocalypse 3.12 Apocalypse 21.2 Philippiens 3.20 Michée 4.1-4.2
27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.Esaïe 54.1-54.5 Ruth 4.14-4.16 Ruth 1.11-1.13 1 Samuel 2.5 Esaïe 49.21
28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.Galates 3.29 Galates 4.23 Romains 4.13-4.18 Romains 9.8-9.9 Actes 3.25
29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.Genèse 21.9 Galates 5.11 1 Thessaloniciens 2.14-2.15 Galates 4.23 Jean 3.5
30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.Jean 8.35 Romains 8.15-8.17 Galates 3.22 Romains 4.3 Genèse 21.10-21.12
31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.Jean 1.12-1.13 1 Jean 3.1-3.2 Hébreux 2.14-2.15 Galates 5.13 Galates 5.1

Cette Bible est dans le domaine public.