Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Juges 4
Bible en Swahili de l’est


1 Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya Bwana. Jérémie 5.3 Juges 2.11 Juges 3.7 Néhémie 9.23-9.30 Juges 3.12
2 Bwana akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake. Juges 4.16 Josué 11.1 Juges 4.13 1 Samuel 12.9 Psaumes 83.9
3 Wana wa Israeli wakamlilia Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini. Juges 1.19 Psaumes 106.42 Juges 3.9 Juges 3.15 Deutéronome 28.33
4 Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Luc 2.36 2 Rois 22.14 Exode 15.20 Michée 6.4 1 Corinthiens 11.5
5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue. Genèse 35.8 Josué 18.25 Jérémie 31.15 1 Samuel 1.1 Josué 18.22
6 Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni? Hébreux 11.32 Juges 8.18 Actes 13.47 Josué 19.37 Josué 19.32
7 Nami nitakuvutia Sisera, amiri wa jeshi lake Yabini, hata mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako. Juges 5.21 1 Rois 18.40 Josué 10.8 Juges 4.14 Psaumes 83.9-83.10
8 Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Matthieu 14.30-14.31 Exode 4.10-4.14
9 Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana Bwana atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. Juges 2.14 Juges 5.24-5.27 2 Samuel 20.21-20.22 1 Samuel 2.30 2 Chroniques 26.18
10 Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye. Juges 5.18 Juges 5.15 Juges 4.14 1 Rois 20.11 1 Samuel 25.27
11 Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni, yaani na wana wa Hobabu, shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mwaloni ulioko Saanaimu, karibu na Kedeshi. Josué 19.33 Juges 1.16 Nombres 10.29 Josué 19.37 Exode 3.1
12 Watu wakamwambia Sisera ya kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu amekwea kwenda mlima wa Tabori. Jérémie 46.18 Josué 19.34 Juges 4.6 Josué 19.12 Psaumes 89.12
13 Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia kenda, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni. Juges 4.2-4.3 Juges 4.7
14 Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo Bwana amemtia Sisera katika mkono wako. Je! Bwana hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata. 2 Samuel 5.24 Deutéronome 9.3 Esaïe 52.12 Genèse 44.4 Michée 2.13
15 Bwana akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu. Josué 10.10 Psaumes 83.9-83.10 Hébreux 11.32 2 Rois 7.6 2 Chroniques 13.15-13.17
16 Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hata Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja. Esaïe 43.17 Psaumes 104.35 Jacques 2.13 Lévitique 26.7-26.8 Romains 2.12
17 Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni. Psaumes 37.35-37.36 Job 40.11-40.12 Proverbes 29.23 Esaïe 57.21 Juges 5.24
18 Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti. 2 Rois 6.19
19 Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika. Juges 5.25-5.26 Esaïe 41.17 Jean 4.7 1 Rois 17.10 Genèse 24.43
20 Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana. 2 Samuel 17.20 Josué 2.3-2.5
21 Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa. Juges 3.31 1 Corinthiens 1.19 Psaumes 3.7 1 Corinthiens 1.27 Juges 3.21
22 Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake. 2 Samuel 17.10-17.15 2 Samuel 17.3
23 Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo. Néhémie 9.24 Psaumes 18.47 Psaumes 81.14 Hébreux 11.33 1 Chroniques 22.18
24 Mkono wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani. 1 Samuel 3.12

Cette Bible est dans le domaine public.