1 Ndipo Yusufu akaja akamwarifu Farao, akasema, Baba yangu, na ndugu zangu, na kondoo zao, na ng’ombe zao, na yote waliyo nayo, wamekuja kutoka nchi ya Kanaani, nao wako katika nchi ya Gosheni.
Genèse 46.31 Genèse 45.10 Genèse 46.28 Hébreux 2.11 Exode 8.22
2 Akatwaa watu watano miongoni mwa nduguze, akawasimamisha mbele ya Farao.
Actes 7.13 Colossiens 1.28 Jude 1.24 2 Corinthiens 4.14
3 Farao akawauliza hao nduguze, Kazi yenu ni nini? Wakamwambia Farao, Watumwa wako tu wachunga wanyama, sisi, na baba zetu.
Genèse 46.33-46.34 Genèse 4.2 2 Thessaloniciens 3.10 Jonas 1.8 Amos 7.14-7.15
4 Wakamwambia Farao, Tumekuja kukaa ugenini katika nchi hii, kwa sababu wanyama wa watumwa wako hawana malisho, maana njaa ni nzito sana katika nchi ya Kanaani. Basi, twakusihi, uturuhusu sisi watumwa wako tukae katika nchi ya Gosheni.
Genèse 46.34 Genèse 15.13 Deutéronome 26.5 Genèse 43.1 Psaumes 105.23
5 Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia;
6 nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu.
Genèse 47.11 Exode 18.21 Exode 18.25 Proverbes 22.29 Genèse 47.4
7 Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao.
Genèse 47.10 2 Samuel 19.39 Matthieu 26.26 Luc 22.19 Genèse 35.27
8 Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi?
9 Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.
Job 14.1 Jacques 4.14 Psaumes 39.12 Psaumes 39.5 Psaumes 119.19
10 Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao.
Genèse 47.7 Genèse 14.19 2 Samuel 19.39 Deutéronome 33.1 Hébreux 7.7
11 Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.
Exode 12.37 Exode 1.11 Genèse 47.6 Jean 14.23 Jean 14.2
12 Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.
Genèse 45.11 Ruth 4.15 1 Timothée 5.8 Genèse 47.1 Marc 7.10-7.13
13 Wala hapakuwa na chakula katika nchi yote, kwa kuwa njaa ilikuwa nzito sana, hata nchi ya Misri, na nchi ya Kanaani zikataabika, kwa sababu ya njaa.
Actes 7.11 Jérémie 9.12 Lamentations 4.9 Jérémie 14.1-14.6 Joël 1.10-1.12
14 Yusufu akakusanya fedha zote zilizoonekana katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, kwa nafaka waliyoinunua. Yusufu akazileta zile fedha nyumbani mwa Farao.
Genèse 41.56 Luc 16.1-16.2 1 Corinthiens 4.2 1 Pierre 4.10 Luc 16.10-16.12
15 Fedha zote zilipokwisha katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, Wamisri wote walimjia Yusufu, wakisema, Tupe sisi chakula, kwa nini tufe mbele ya macho yako? Maana fedha zetu zimekwisha.
Genèse 47.18-47.19 Matthieu 6.11 Juges 8.8 Psaumes 37.3 1 Samuel 25.8
16 Yusufu akasema, Toeni wanyama wenu, nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu, kama fedha zenu zimekwisha.
Daniel 6.5-6.7 Philippiens 4.8 1 Corinthiens 10.32 Colossiens 4.5 Proverbes 12.17
17 Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng’ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule.
Exode 9.3 Esaïe 31.1 Matthieu 6.24 1 Rois 10.28 Job 2.4
18 Na mwaka ule ulipokwisha wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu ya kwamba fedha zetu zimekwisha, na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu, hakikusalia kitu mbele ya bwana wetu, ila miili yetu na nchi zetu.
Jérémie 38.9 2 Rois 6.26
19 Kwa nini tufe mbele ya macho yako, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu kwa chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao; kisha utupe mbegu, tuishi wala tusife, wala nchi yetu isipotee.
Néhémie 5.2-5.3 Lamentations 1.11 Lamentations 5.9 Lamentations 5.6 Matthieu 16.26
20 Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri; maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake; kwa sababu njaa ilikuwa imewazidi sana, nchi ikawa mali yake Farao.
21 Akawahamisha hao watu, akawaweka katika miji, tangu upande huu wa Misri hata upande huu.
Genèse 41.48
22 Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
Esdras 7.24 Deutéronome 12.19 2 Samuel 8.18 Genèse 41.50 Josué 21.1-21.45
23 Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi.
Genèse 41.27 Psaumes 112.5 Psaumes 41.1 Esaïe 55.10 Psaumes 107.36-107.37
24 Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu.
Genèse 41.34 1 Samuel 8.15-8.17 Psaumes 112.5 Lévitique 27.32 Psaumes 41.1
25 Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.
Genèse 33.15 Ruth 2.13 Genèse 50.20 Genèse 41.45 Genèse 6.19
26 Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Genèse 47.22 Ezéchiel 7.24
27 Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana.
Exode 1.7 Genèse 46.3 Actes 7.17 Deutéronome 26.5 Genèse 26.4
28 Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, basi siku za miaka ya maisha yake Yakobo ilikuwa miaka mia moja na arobaini na saba.
Genèse 37.2 Psaumes 90.12 Genèse 47.8-47.9 Psaumes 119.84 Psaumes 90.10
29 Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri.Deutéronome 31.14 Genèse 24.49 Genèse 24.2 1 Rois 2.1 Genèse 50.24-50.25
30 Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.
Genèse 49.29-49.32 Genèse 25.9 Genèse 23.19 Néhémie 2.5 Genèse 50.5-50.14
31 Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda.
1 Rois 1.47 Hébreux 11.21 Genèse 24.3 Genèse 47.29 Genèse 24.26