25 Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia; 2 Chroniques 16.2 2 Rois 18.15 2 Chroniques 26.10 Genèse 41.48 Jérémie 41.8 26 na juu ya hao wenye kazi ya shamba kuilima ardhi alikuwa Ezri mwana wa Kelubu; 27 na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi; 28 na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi; 1 Rois 10.27 2 Chroniques 1.15 1 Rois 20.27 1 Rois 4.7 29 na juu ya makundi ya ng’ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai; 1 Chroniques 5.16 Esaïe 65.10 30 na juu ya ngamia alikuwa Obili, Mwishmaeli; na juu ya punda alikuwa Yedeya, Mmeronothi; Job 1.3 Genèse 47.6 31 na juu ya makundi ya kondoo alikuwa Yazizi, Mhagri. Hao wote walikuwa maakida wa akiba alizokuwa nazo mfalme Daudi. 1 Chroniques 5.10 32 Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme; 2 Samuel 21.21 1 Chroniques 11.11 2 Samuel 13.3 33 na Ahithofeli alikuwa mshauri wake mfalme; na Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki yake mfalme; 2 Samuel 15.12 2 Samuel 15.37 2 Samuel 15.32 Psaumes 55.13 2 Samuel 16.16-16.17 34 na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu. 1 Chroniques 11.6 1 Rois 1.7 1 Chroniques 27.5