Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 39
Bible en Swahili de l’est


1 Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu? 1 Samuel 24.2 Psaumes 104.18 Psaumes 29.9 Jérémie 14.5 Deutéronome 14.5
2 Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao? Jérémie 2.24
3 Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao. 4 Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena. 5 Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu? Job 24.5 Job 6.5 Job 11.12 Psaumes 104.11 Jérémie 2.24
6 Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake. Psaumes 107.34 Jérémie 2.24 Deutéronome 29.23 Jérémie 17.6 Job 24.5
7 Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Job 3.18 Esaïe 31.4 Exode 5.13-5.16 Esaïe 58.3 Job 39.18
8 Upana wa milima ni malisho yake, Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi. Genèse 1.29-1.30 Psaumes 145.15-145.16 Job 40.20-40.22 Job 40.15 Psaumes 104.27-104.28
9 Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako? Nombres 23.22 Deutéronome 33.17 Psaumes 92.10 Psaumes 22.21 Esaïe 1.3
10 Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako? Job 41.5 Job 39.7 Osée 10.10-10.11 Job 39.5 Michée 1.13
11 Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako? Psaumes 20.7 Psaumes 147.10 Esaïe 30.6 Genèse 42.26 Esaïe 30.16
12 Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria? Amos 2.13 Matthieu 3.2 Proverbes 3.16 Matthieu 13.30 Néhémie 13.15
13 Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma? Zacharie 5.9 Jérémie 8.7 1 Rois 10.22 Lévitique 11.19 Job 30.29
14 Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi, Na kuyatia moto mchangani, 15 Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja, Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga. 16 yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake; Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu; Lamentations 4.3 Ecclésiaste 10.15 1 Rois 3.26-3.27 Romains 1.31 2 Rois 6.28-6.29
17 Kwa sababu Mungu amemnyima akili, Wala hakumpa fahamu. Job 35.11 Job 17.4 Esaïe 19.11-19.14 2 Chroniques 32.31 Deutéronome 2.30
18 Wakati anapojiinua juu aende, Humdharau farasi na mwenye kumpanda. Job 39.7 Job 5.22 Job 39.22 2 Rois 19.21 Job 41.29
19 Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake? Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo? Psaumes 147.10 Job 39.25 Marc 3.17 Psaumes 93.1 Psaumes 104.1
20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha. Jérémie 8.16 Job 41.20-41.21 Joël 2.5
21 Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake; Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha. Jérémie 8.6 Jérémie 9.23 Juges 5.22 Psaumes 19.5 1 Samuel 17.42
22 Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai; Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga. Job 39.18 Job 41.33 Job 39.16
23 Podo humpigia makelele, Mkuki ung’aao na fumo. Job 41.26-41.29
24 Huimeza nchi kwa ukali wake na ghadhabu; Wala hasimami kwa sauti ya baragumu. Habakuk 1.8-1.9 Luc 24.41 Job 9.16 Job 37.20 Jérémie 4.19
25 Kila ipigwapo baragumu yeye husema, Aha! Naye husikia harufu ya vita toka mbali, Mshindo wa maakida, na makelele. Ezéchiel 26.2 Psaumes 70.3 Ezéchiel 36.2
26 Je! Mwewe huruka juu kwa akili zako, Na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini? Lévitique 16.11 Jérémie 8.7 Cantique 2.12 Deutéronome 14.15
27 Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake mahali pa juu? Abdias 1.4 Jérémie 49.16 Psaumes 103.5 Exode 19.4 Lévitique 11.13
28 Hukaa jabalini, ndiko kwenye malazi yake, Juu ya genge la jabali, na ngomeni. 1 Samuel 14.4
29 Toka huko yeye huchungulia mawindo; Macho yake huyaangalia toka mbali. Job 9.26
30 Makinda yake nayo hufyonza damu; Na kwenye maiti ndiko aliko. Matthieu 24.28 Luc 17.37 Ezéchiel 39.17-39.19

Cette Bible est dans le domaine public.