Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 1.4
Bible en Swahili de l’est


1 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.Proverbes 10.1 1 Rois 4.31-4.32 Ecclésiaste 12.9 Proverbes 25.1 2 Samuel 12.24-12.25
2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;Proverbes 7.4 Deutéronome 4.5-4.6 Proverbes 17.16 Proverbes 4.5-4.7 Proverbes 8.5
3 kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili.Proverbes 2.1-2.9 1 Rois 3.28 Job 22.22 Proverbes 8.10-8.11
4 Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari;Proverbes 8.5 Proverbes 8.12 Proverbes 8.32 2 Timothée 2.22 Proverbes 3.21
5 mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.Proverbes 9.9 Psaumes 119.98-119.100 Job 34.16 1 Corinthiens 10.15 Proverbes 12.1
6 Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.Psaumes 78.2 Psaumes 49.4 Marc 4.11 Actes 8.30-8.31 Matthieu 13.10-13.17
7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.Job 28.28 Proverbes 9.10 Ecclésiaste 12.13 Proverbes 15.33 Psaumes 111.10-112.1
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,Proverbes 6.20 1 Samuel 2.25 Proverbes 5.1-5.2 Proverbes 4.1-4.4 Proverbes 2.1
9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.Proverbes 4.9 Genèse 41.42 Daniel 5.29 Proverbes 3.22 Daniel 5.16
10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.Ephésiens 5.11 Proverbes 16.29 Psaumes 50.18 Psaumes 1.1 Deutéronome 13.8
11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;Proverbes 1.18 Proverbes 12.6 Jérémie 5.26 Psaumes 35.7 Jean 15.25
12 Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.Psaumes 28.1 Psaumes 124.3 Psaumes 143.7 Jérémie 51.34 Nombres 16.30-16.33
13 Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka.Jérémie 22.16-22.17 Aggée 2.9 Esaïe 10.13-10.14 Proverbes 1.19 Luc 12.15
14 Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika. 15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.Psaumes 119.101 Psaumes 1.1 Proverbes 4.27 Proverbes 4.14-4.15 Psaumes 26.4-26.5
16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.Proverbes 6.18 Esaïe 59.7 Proverbes 4.16 Romains 3.5
17 Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege ye yote.Job 35.11 Esaïe 1.3 Proverbes 7.23 Jérémie 8.7
18 Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.Matthieu 27.4-27.5 Psaumes 9.16 Proverbes 28.17 Proverbes 9.17-9.18 Psaumes 55.23
19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.Proverbes 15.27 Habakuk 2.9 Michée 2.1-2.3 Actes 8.19-8.20 1 Timothée 3.3
20 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja;Proverbes 9.3 1 Corinthiens 1.24 Colossiens 2.3 1 Corinthiens 1.30 Jean 7.37
21 Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.Actes 5.20 Matthieu 10.27 Jean 18.20 Proverbes 9.3 Matthieu 13.2
22 Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?Proverbes 1.29 Proverbes 5.12 Psaumes 1.1 Proverbes 3.34 Proverbes 9.16-9.18
23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.Esaïe 32.15 Joël 2.28 Ezéchiel 33.11 Zacharie 12.10 Ezéchiel 18.27-18.30
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;Esaïe 65.12 Romains 10.21 Jérémie 7.13 Esaïe 66.4 Ezéchiel 8.18
25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu;Proverbes 1.30 Luc 7.30 Psaumes 81.11 Proverbes 12.1 Psaumes 107.11
26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;Psaumes 2.4 Proverbes 10.24 Psaumes 37.13 Luc 14.24 Juges 10.14
27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.Proverbes 3.25-3.26 Romains 2.9 Luc 21.34-21.35 Psaumes 58.9 Proverbes 10.24-10.25
28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.Jérémie 11.11 Job 27.9 Jacques 4.3 Michée 3.4 Jérémie 14.12
29 Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.Proverbes 1.22 Esaïe 27.11 Proverbes 6.23 Psaumes 50.16-50.17 Jean 3.20
30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.Proverbes 1.25 Psaumes 81.11 Psaumes 119.173 Luc 14.18-14.20 Jérémie 8.9
31 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.Job 4.8 Proverbes 14.14 Jérémie 6.19 Proverbes 22.8 Galates 6.7-6.8
32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.Jean 3.36 Proverbes 8.36 Jérémie 2.19 Deutéronome 32.15-32.44 Jérémie 48.11-48.12
33 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.Psaumes 25.12-25.13 Esaïe 26.3 Proverbes 9.11 Luc 21.9 Psaumes 112.7-112.8

Cette Bible est dans le domaine public.