Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 16.31
Bible en Swahili de l’est


1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.Proverbes 19.21 Proverbes 16.9 Proverbes 20.24 Matthieu 10.19-10.20 Philippiens 2.13
2 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu.Proverbes 21.2 1 Samuel 16.7 Proverbes 30.12 Luc 16.15 Proverbes 24.12
3 Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.Psaumes 37.4-37.5 Proverbes 3.6 Psaumes 55.22 Philippiens 4.6 1 Pierre 5.7
4 Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.Romains 9.22 Esaïe 43.21 1 Pierre 2.8 Esaïe 43.7 Romains 11.36
5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.Proverbes 6.16-6.17 Proverbes 8.13 Proverbes 11.21 Jacques 4.6 Romains 2.8-2.9
6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.Proverbes 14.16 Job 28.28 Daniel 4.27 Luc 11.41 Proverbes 8.13
7 Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.Genèse 33.4 1 Jean 3.22 Jérémie 15.11 2 Chroniques 17.10 Hébreux 13.21
8 Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.Psaumes 37.16 Proverbes 15.16 Michée 6.10 Jérémie 17.11 1 Timothée 6.6-6.9
9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.Proverbes 16.1 Proverbes 19.21 Psaumes 37.23 Proverbes 20.24 Jérémie 10.23
10 Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu.Esaïe 32.1-32.2 2 Samuel 23.3-23.4 Jérémie 23.5-23.6 Psaumes 99.4 Psaumes 45.6-45.7
11 Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya Bwana; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake.Proverbes 11.1 Lévitique 19.35-19.36 Osée 12.7 Ezéchiel 45.10 Amos 8.5
12 Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki.Proverbes 25.5 Proverbes 29.14 Proverbes 28.9 Psaumes 99.4 Deutéronome 25.16
13 Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa.Proverbes 14.35 Proverbes 22.11 Psaumes 101.5-101.7
14 Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza.Proverbes 19.12 Proverbes 20.2 Ecclésiaste 10.4 2 Corinthiens 5.20 Actes 12.20
15 Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika.Job 29.23-29.24 Psaumes 72.6 Osée 6.3 Psaumes 30.5 Psaumes 4.6
16 Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.Proverbes 8.19 Proverbes 8.10-8.11 Job 28.13-28.28 Luc 12.21 Ecclésiaste 7.12
17 Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.Esaïe 35.8 Apocalypse 3.10 Matthieu 24.13 Proverbes 10.9 Tite 2.10-2.14
18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.Proverbes 11.2 Proverbes 18.12 Esaïe 2.11-2.12 Abdias 1.3-1.4 Proverbes 29.23
19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.Esaïe 57.15 Exode 15.9 Luc 1.51-1.53 Proverbes 29.23 Matthieu 5.3
20 Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye Bwana ana heri.Psaumes 2.12 Proverbes 19.8 Psaumes 34.8 Proverbes 13.15 Esaïe 26.3-26.4
21 Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu.Proverbes 16.23-16.24 Esaïe 50.4 Jean 7.46 Luc 4.22 Proverbes 15.7
22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.Luc 6.39-6.40 Proverbes 13.14 Proverbes 10.11 Jean 5.24 Jean 6.68
23 Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.Proverbes 15.28 Matthieu 12.34-12.35 Colossiens 3.16 Psaumes 45.1 Psaumes 37.30-37.31
24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.Proverbes 24.13-24.14 Psaumes 19.10 Proverbes 25.11-25.12 Psaumes 119.103 Proverbes 4.22
25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.Proverbes 14.12 Actes 26.9 Proverbes 12.15 2 Corinthiens 13.5 Proverbes 12.26
26 Nafsi yake mfanya kazi hujifanyia kazi; Maana kinywa chake humtia bidii.Ecclésiaste 6.7 2 Thessaloniciens 3.8-3.12 Proverbes 14.23 1 Thessaloniciens 4.11-4.12 Proverbes 9.12
27 Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara; Katika midomo yake mna moto uteketezao.Jacques 3.6 2 Samuel 20.1 Habakuk 2.13 Psaumes 17.14-17.15 Psaumes 52.2-52.4
28 Mtu mshupavu huondokesha fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.Proverbes 17.9 Proverbes 15.18 Proverbes 18.8 Proverbes 6.19 Proverbes 30.33
29 Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema.Proverbes 1.10-1.14 1 Samuel 19.11 Néhémie 6.13 1 Samuel 22.7-22.9 1 Samuel 19.17
30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.Michée 7.3 Matthieu 27.23-27.26 Proverbes 10.10 Proverbes 16.27 Jean 3.20
31 Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.Proverbes 20.29 Lévitique 19.32 1 Samuel 12.2-12.5 Proverbes 3.1-3.2 Genèse 47.7-47.10
32 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.Proverbes 15.18 Proverbes 14.29 Proverbes 19.11 Jacques 1.19 Romains 12.21
33 Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za Bwana.Proverbes 18.18 Jonas 1.7 Néhémie 11.1 1 Samuel 14.41-14.42 Josué 18.10

Cette Bible est dans le domaine public.