Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 4.2
Bible en Swahili de l’est


1 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.Proverbes 1.8 Psaumes 34.11 1 Thessaloniciens 2.11-2.12 Hébreux 2.1 Proverbes 5.1
2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.Deutéronome 32.2 Proverbes 8.6-8.9 Job 33.3 Psaumes 89.30-89.32 1 Chroniques 28.9
3 Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.1 Chroniques 22.5 1 Chroniques 29.1 1 Rois 1.13-1.17 Romains 12.16 Zacharie 12.10
4 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.Proverbes 7.2 Ephésiens 6.4 1 Chroniques 28.9 Esaïe 55.3 Proverbes 3.1
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.Psaumes 119.157 Proverbes 2.2-2.4 Psaumes 119.51 2 Chroniques 34.2 Proverbes 23.23
6 Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda.2 Thessaloniciens 2.10 Proverbes 2.10-2.12 Ephésiens 3.17 Proverbes 4.21-4.22
7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.Matthieu 13.44-13.46 Philippiens 3.8 Proverbes 23.23 Luc 12.20 Proverbes 21.6
8 Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia.1 Samuel 2.30 Daniel 12.3 1 Rois 3.5-3.13 Proverbes 22.4 Proverbes 3.35
9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.Proverbes 1.9 Proverbes 16.31 1 Timothée 2.9-2.10 Hébreux 2.7-2.9 Esaïe 28.5
10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.Proverbes 3.2 Proverbes 2.1 Deutéronome 6.2 Jérémie 9.20 Proverbes 19.20
11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.Psaumes 23.3 Actes 13.10 1 Samuel 12.23-12.24 Proverbes 8.9 Proverbes 4.4
12 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.Proverbes 3.23 Psaumes 18.36 2 Samuel 22.37 Job 18.7-18.8 Psaumes 91.11-91.12
13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.Proverbes 3.18 Proverbes 3.22 Proverbes 23.23 Hébreux 2.1 Cantique 3.4
14 Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya.Proverbes 1.15 Psaumes 1.1 1 Corinthiens 15.33 Proverbes 1.10 Proverbes 13.20
15 Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako.Proverbes 6.5 Job 22.23 1 Thessaloniciens 5.22 Ephésiens 5.11 Job 11.14
16 Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.Psaumes 36.4 Michée 2.1 2 Pierre 2.14 Esaïe 57.20 Proverbes 1.16
17 Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya jeuri.Psaumes 14.4 Ezéchiel 22.25-22.29 Michée 3.5 Matthieu 23.13 Jacques 5.4-5.5
18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.Job 11.17 Philippiens 2.15 2 Samuel 23.4 Psaumes 84.7 Jean 8.12
19 Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.Esaïe 59.9-59.10 Jean 12.35 Jérémie 23.12 Job 18.5-18.6 1 Samuel 2.9
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.Proverbes 5.1 Esaïe 55.3 Proverbes 7.1 Matthieu 17.5 Psaumes 78.1
21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.Proverbes 3.21 Proverbes 2.1 Proverbes 3.3 Psaumes 40.8 Proverbes 7.1-7.2
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.Proverbes 3.8 Proverbes 12.18 Proverbes 4.10 Proverbes 4.4 Jérémie 33.6
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.Luc 6.45 Matthieu 12.34-12.35 Marc 7.21-7.23 Psaumes 139.23-139.24 Jérémie 17.9
24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.Jacques 1.26 Jacques 1.21 Proverbes 8.8 Ephésiens 4.25-4.31 1 Pierre 2.1
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.Proverbes 23.33 Matthieu 6.22 Psaumes 119.37
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;2 Thessaloniciens 3.3 1 Thessaloniciens 3.13 Psaumes 119.5 Proverbes 5.6 Psaumes 37.23
27 Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.Deutéronome 5.32 Deutéronome 28.14 Josué 1.7 Deutéronome 12.32 Esaïe 1.16

Cette Bible est dans le domaine public.