Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 24.20
Bible en Swahili de l’est


1 Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.Nahum 2.10 Esaïe 42.15 Ezéchiel 12.20 Ezéchiel 5.2 Esaïe 24.20
2 Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.Osée 4.9 Ezéchiel 7.12-7.13 Ephésiens 6.8-6.9 Esaïe 9.14-9.17 Deutéronome 23.19-23.20
3 Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo.Esaïe 24.1 Esaïe 6.11 2 Chroniques 36.21 Jérémie 13.15 Michée 4.4
4 Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.Osée 4.3 Esaïe 33.9 Esaïe 2.11-2.12 Jérémie 12.4 Esaïe 3.26
5 Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.Romains 8.20-8.21 Nombres 35.33-35.34 Daniel 7.25 Ezéchiel 20.24 Esaïe 1.2-1.5
6 Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.Zacharie 5.3-5.4 Malachie 4.1 Malachie 3.9 Josué 23.15-23.16 Deutéronome 4.27
7 Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua.Esaïe 16.10 Joël 1.10-1.12 Esaïe 16.8 Esaïe 32.9-32.13 Osée 9.1-9.2
8 Sauti ya furaha ya matoazi inakoma; kelele yao wafurahio imekwisha; furaha ya kinubi inakoma.Osée 2.11 Jérémie 7.34 Ezéchiel 26.13 Apocalypse 18.22 Jérémie 25.10
9 Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao.Esaïe 5.22 Ecclésiaste 9.7 Esaïe 5.11-5.12 Ephésiens 5.18-5.19 Amos 8.10
10 Mji wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote.Michée 3.12 2 Rois 25.4 Esaïe 24.12 Luc 19.43 Esaïe 27.10
11 Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.Esaïe 16.10 Esaïe 9.19 Lamentations 5.14-5.15 Proverbes 31.6 Joël 1.15
12 Ndani ya mji umebaki ukiwa, na lango lake limepigwa kwa uharibifu.Lamentations 1.4 Jérémie 9.11 Matthieu 22.7 Lamentations 5.18 Michée 1.12
13 Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.Esaïe 1.9 Apocalypse 3.4 Jérémie 44.28 Apocalypse 11.2-11.3 Ezéchiel 14.22-14.23
14 Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga kelele toka baharini.Esaïe 25.1 Jérémie 30.19 Sophonie 3.14-3.20 Esaïe 52.7-52.9 Zacharie 2.10
15 Basi, mtukuzeni Bwana katika mashariki, litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.Malachie 1.11 Esaïe 49.1 Esaïe 60.9 Esaïe 51.5 Esaïe 42.10
16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.Esaïe 21.2 Esaïe 33.1 Jérémie 5.11 Jérémie 3.20 Esaïe 10.16
17 Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.Jérémie 48.43-48.44 Ezéchiel 14.21 Lévitique 26.21-26.22 1 Rois 19.17 Amos 5.19
18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.Psaumes 18.7 Genèse 7.11 Genèse 19.24 Job 20.24 Amos 5.19
19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.Apocalypse 20.11 Nahum 1.5 Esaïe 24.1-24.5 Jérémie 4.23-4.28 Habakuk 3.6
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.Esaïe 19.14 Daniel 11.19 Esaïe 29.9 Amos 8.14 Osée 4.1-4.5
21 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;Psaumes 76.12 Esaïe 10.12 Ezéchiel 38.1-38.23 Zacharie 14.12-14.19 Apocalypse 6.14-6.17
22 nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.Zacharie 9.11 Jérémie 38.6-38.13 Esaïe 42.22 Josué 10.16-10.17 Ezéchiel 38.8
23 Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.Esaïe 13.10 Esaïe 60.19 Michée 4.7 Hébreux 12.22 Apocalypse 21.23

Cette Bible est dans le domaine public.