Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 26
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanzo wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili lilitoka kwa Bwana, kusema, Jérémie 27.1 2 Chroniques 36.4-36.5 Jérémie 35.1 2 Rois 23.34-23.36 Jérémie 25.1
2 Bwana asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja. Deutéronome 4.2 Jérémie 19.14 Actes 20.27 Jérémie 1.17 Matthieu 28.20
3 Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao. Jérémie 36.3 Jérémie 18.7-18.10 Esaïe 1.16-1.19 Jonas 4.2 Jérémie 36.7
4 Nawe utawaambia, Bwana asema hivi, Kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, niliyoiweka mbele yenu, 1 Rois 9.6 Esaïe 1.20 Jérémie 44.10 Néhémie 9.26-9.30 Deutéronome 31.16-31.18
5 kuyasikiliza maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza; Jérémie 25.3-25.4 Esdras 9.11 Jérémie 7.13 2 Rois 9.7 Jérémie 7.25
6 basi, nitafanya nyumba hii kuwa kama Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa taifa zote za dunia. Jérémie 24.9 2 Rois 22.19 Jérémie 25.18 Esaïe 65.15 Josué 18.1
7 Na makuhani, na manabii, na watu wote, wakamsikia Yeremia, hapo aliposema maneno haya katika nyumba ya Bwana. Michée 3.11 Jérémie 5.31 Actes 5.17 Ezéchiel 22.25-22.26 Jérémie 23.11-23.15
8 Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote Bwana aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa. Lamentations 4.13-4.14 Matthieu 21.35-21.39 Apocalypse 18.24 Matthieu 23.31-23.35 Jérémie 11.19-11.21
9 Kwa nini umetabiri kwa jina la Bwana, ukisema, Nyumba hii itakuwa kama Shilo, na mji huu utakuwa ukiwa, hautakaliwa na mtu? Watu wote wakamkusanyikia Yeremia katika nyumba ya Bwana. Jean 8.59 Michée 2.6 Actes 4.17-4.19 Actes 21.30 Actes 19.24-19.32
10 Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa Bwana; wakaketi, hapo watu waingiapo katika lango jipya la nyumba ya Bwana. Jérémie 36.10 2 Rois 15.35 Jérémie 34.19 Ezéchiel 22.27 Ezéchiel 22.6
11 Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu amestahili kufa, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu. Jérémie 38.4 Matthieu 26.66 Deutéronome 18.20 Actes 6.11-6.14 Actes 25.2-25.13
12 Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, Bwana ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia. Actes 4.19 Actes 5.29 Jérémie 26.15 Jérémie 26.2 Jérémie 1.17-1.18
13 Basi sasa, tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, mkaisikilize sauti ya Bwana, Mungu wenu; naye Bwana atayaghairi mabaya aliyoyanena juu yenu. Jérémie 26.3 Jonas 4.2 Jérémie 35.15 Jonas 3.9 Joël 2.14
14 Lakini kwangu mimi, tazama, mimi nipo hapa mikononi mwenu; nitendeni myaonayo kuwa mema na haki mbele ya macho yenu. Jérémie 38.5 Josué 9.25 Daniel 3.16 2 Samuel 15.26
15 Lakini jueni yakini ya kuwa, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia. Nombres 35.33 Jérémie 7.6 Proverbes 6.17 Matthieu 26.25 Genèse 4.10
16 Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la Bwana Mungu wetu. Actes 23.29 Actes 5.34-5.39 Actes 23.9 Jérémie 36.19 Jérémie 36.25
17 Ndipo watu kadha wa kadha miongoni mwa wazee wa nchi wakaondoka, wakanena na mkutano wa watu, wakisema, Actes 5.34 Michée 1.1
18 Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, Bwana wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni. Néhémie 4.2 Jérémie 17.3 Michée 3.12-4.1 Jérémie 9.11 Zacharie 8.3
19 Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha Bwana, na kumwomba Bwana awafadhili; naye Bwana akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya roho zetu. 2 Samuel 24.16 Exode 32.14 Esaïe 37.15-37.20 2 Chroniques 32.25-32.26 Esaïe 37.1
20 Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la Bwana, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia; 1 Samuel 7.2 Josué 9.17 1 Samuel 6.21 Josué 15.60 Josué 18.14
21 na Yehoyakimu, mfalme, na mashujaa wake wote, na wakuu wake wote, waliposikia maneno yake, mfalme akataka kumwua; lakini Uria alipopata habari, aliogopa, akakimbia akaenda Misri. Matthieu 10.23 Jérémie 36.26 Matthieu 14.5 2 Chroniques 16.10 Psaumes 119.109
22 Basi, mfalme Yehoyakimu akatuma watu waende Misri, Elnathani, mwana wa Akbori, na watu wengine pamoja naye, kwenda Misri; 2 Rois 22.14 2 Rois 22.12 Jérémie 36.12 Jérémie 36.25 Psaumes 12.8
23 wakamtoa Uria katika Misri, wakamleta kwa Yehoyakimu, mfalme; naye akamwua kwa upanga, akamtupa yule maiti katika makaburi ya watu wasio na cheo. Jérémie 2.30 Ezéchiel 19.6 Apocalypse 11.7 Matthieu 14.10 Jérémie 22.19
24 Lakini mkono wa Ahikamu, mwana wa Shafani, alikuwa pamoja na Yeremia, wasimtie katika mikono ya watu auawe. Jérémie 40.5-40.7 Jérémie 1.18-1.19 2 Rois 22.12-22.14 1 Rois 18.4 Jérémie 39.14

Cette Bible est dans le domaine public.