Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Ezéchiel 45.18 Bible en Swahili de l’est
Territoire réservé à l’Éternel et au prince
1 Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea Bwana toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote. Ezéchiel 48.29 Nombres 34.13 Zacharie 14.20-14.21 Lévitique 25.23 Josué 13.6 2 Katika hiyo itakuwako sehemu kwa mahali patakatifu, urefu wake mia tano, na upana wake mia tano, mraba pande zote; na dhiraa ishirini kwa viunga vyake pande zote. Ezéchiel 42.16-42.20 Ezéchiel 27.28 3 Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana. Ezéchiel 48.10 4 Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia Bwana; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu. Nombres 16.5 Ezéchiel 40.45 Ezéchiel 43.19 Ezéchiel 45.1 Ezéchiel 48.10-48.11 5 Tena urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi, ni sehemu ya Walawi, wahudumu wa nyumba, iwe milki yao wenyewe kwa vyumba ishirini. Ezéchiel 48.13 1 Corinthiens 9.13-9.14 1 Chroniques 9.26-9.33 Ezéchiel 48.20 Ezéchiel 48.10 6 Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake ishirini na tano elfu, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli. Ezéchiel 48.15-48.18 Ezéchiel 48.30-48.35 7 Na sehemu itakayokuwa ya mkuu itakuwa upande huu, na upande huu, wa toleo takatifu, na wa milki ya mji, kulikabili toleo takatifu, na kuikabili milki ya mji, upande wa magharibi kuelekea magharibi, na upande wa mashariki kuelekea mashariki; na kwa urefu wake sawasawa na sehemu mojawapo, toka mpaka wa magharibi hata mpaka wa mashariki. Ezéchiel 48.21 Ezéchiel 37.24 Ezéchiel 46.16-46.18 Ezéchiel 34.24 Luc 1.32-1.33 8 Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao. Ezéchiel 46.18 Ezéchiel 22.27 Jérémie 23.5 Esaïe 11.3-11.5 Josué 11.23