Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 45
Bible en Swahili de l’est


1 Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea Bwana toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote. Ezéchiel 48.29 Nombres 34.13 Zacharie 14.20-14.21 Lévitique 25.23 Josué 13.6
2 Katika hiyo itakuwako sehemu kwa mahali patakatifu, urefu wake mia tano, na upana wake mia tano, mraba pande zote; na dhiraa ishirini kwa viunga vyake pande zote. Ezéchiel 42.16-42.20 Ezéchiel 27.28
3 Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana. Ezéchiel 48.10
4 Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia Bwana; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu. Nombres 16.5 Ezéchiel 40.45 Ezéchiel 43.19 Ezéchiel 45.1 Ezéchiel 48.10-48.11
5 Tena urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi, ni sehemu ya Walawi, wahudumu wa nyumba, iwe milki yao wenyewe kwa vyumba ishirini. Ezéchiel 48.13 1 Corinthiens 9.13-9.14 1 Chroniques 9.26-9.33 Ezéchiel 48.20 Ezéchiel 48.10
6 Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake ishirini na tano elfu, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli. Ezéchiel 48.15-48.18 Ezéchiel 48.30-48.35
7 Na sehemu itakayokuwa ya mkuu itakuwa upande huu, na upande huu, wa toleo takatifu, na wa milki ya mji, kulikabili toleo takatifu, na kuikabili milki ya mji, upande wa magharibi kuelekea magharibi, na upande wa mashariki kuelekea mashariki; na kwa urefu wake sawasawa na sehemu mojawapo, toka mpaka wa magharibi hata mpaka wa mashariki. Ezéchiel 48.21 Ezéchiel 37.24 Ezéchiel 46.16-46.18 Ezéchiel 34.24 Luc 1.32-1.33
8 Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao. Ezéchiel 46.18 Ezéchiel 22.27 Esaïe 11.3-11.5 Josué 11.23 Ezéchiel 19.7
9 Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang’anyi; fanyeni hukumu na haki; ondoeni kutoza kwa nguvu kwenu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU. Zacharie 8.16 Ezéchiel 44.6 Jérémie 22.3 Néhémie 5.1-5.13 Esaïe 1.17
10 Mtakuwa na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki. Amos 8.4-8.6 Michée 6.10-6.11 Proverbes 11.1 Proverbes 16.11 Lévitique 19.35-19.36
11 Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri. Esaïe 5.10
12 Nayo shekeli itakuwa gera ishirini; shekeli tano zitakuwa shekeli tano, shekeli kumi zitakuwa kumi, na shekeli hamsini zitakuwa mane yenu. Exode 30.13 Lévitique 27.25 Nombres 3.47
13 Toleo mtakalotoa ni hili; sehemu ya sita ya efa katika homeri moja ya ngano, nanyi mtatoa sehemu ya sita ya efa katika homeri ya shayiri; 14 na sehemu ya mafuta iliyoamriwa, katika bathi ya mafuta, itakuwa sehemu ya kumi ya bathi katika kori moja, ambayo ni bathi kumi, yaani homeri; maana bathi kumi ni homeri moja; 15 na mwana-kondoo mmoja wa kundi katika mia mbili, katika malisho ya Israeli yenye maji; kwa sadaka ya unga, na kwa sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka za amani, ili kuwafanyia upatanisho, asema Bwana MUNGU. Lévitique 1.4 Lévitique 6.30 Colossiens 1.21 Proverbes 3.9-3.10 2 Corinthiens 5.19-5.21
16 Watu wote wa nchi watatoa toleo hili kwa ajili ya mkuu katika Israeli. Exode 30.14-30.15 Esaïe 16.1
17 Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli. 2 Chroniques 31.3 Ezéchiel 46.4-46.12 Esaïe 66.23 Nombres 28.1-28.29 1 Rois 8.63-8.64
18 Bwana MUNGU asema hivi; Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng’ombe mchanga mume mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu. Lévitique 16.16 Lévitique 16.33 Lévitique 22.20 Exode 12.2 Hébreux 9.14
19 Na kuhani atatwaa baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi, na kuitia juu ya miimo ya milango ya nyumba, na juu ya pembe nne za daraja ya madhabahu, na juu ya miimo ya lango la ua wa ndani. Ezéchiel 43.20 Lévitique 16.18-16.20 Ezéchiel 43.14 Ezéchiel 43.17
20 Nawe utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba upatanisho. Ezéchiel 45.18 Lévitique 4.27-4.35 Ezéchiel 45.15 Psaumes 19.12 Lévitique 16.20
21 Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na Pasaka, sikukuu ya siku saba; mkate usiotiwa chachu utaliwa. Lévitique 23.5-23.8 Exode 12.1-12.51 Deutéronome 16.1-16.8 1 Corinthiens 5.7-5.8 Nombres 28.16-28.25
22 Na siku hiyo mkuu atatengeneza ng’ombe kuwa sadaka ya dhambi, kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu wote wa nchi. Lévitique 4.14 Matthieu 26.26-26.28 Matthieu 20.28 2 Corinthiens 5.21
23 Tena, katika zile siku saba za sikukuu atamtengenezea Bwana sadaka ya kuteketezwa, ng’ombe saba na kondoo waume saba wakamilifu, kila siku kwa muda wa siku saba, na beberu mmoja kila siku kuwa sadaka ya dhambi. Job 42.8 Lévitique 23.8 Nombres 23.1-23.2 Nombres 29.11-29.38 Hébreux 10.8-10.12
24 Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng’ombe, na efa moja kwa kondoo mume, na hini moja ya mafuta kwa efa moja; Ezéchiel 46.5-46.7 Nombres 28.12-28.15
25 katika mwezi wa saba, siku ya kumi na tano ya mwezi, katika sikukuu atafanya vivyo hivyo kwa muda wa siku saba; sadaka ya dhambi vivyo hivyo, na sadaka ya kuteketezwa vivyo hivyo, na sadaka ya unga vivyo hivyo, na mafuta vivyo hivyo. Nombres 29.12-29.38 2 Chroniques 5.3 Lévitique 23.33-23.43 2 Chroniques 7.8-7.10 Zacharie 14.16-14.19

Cette Bible est dans le domaine public.