Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Apocalypse 2
Bible en Swahili de l’est


1 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Apocalypse 1.16 Apocalypse 1.11-1.13 Apocalypse 1.20 Apocalypse 3.1 Apocalypse 2.8
2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 1 Jean 4.1 2 Pierre 2.1-2.3 1 Thessaloniciens 5.21 Apocalypse 3.8 Apocalypse 3.15
3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Hébreux 10.36 2 Corinthiens 4.1 Hébreux 6.12 Apocalypse 1.9 2 Pierre 1.6
4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Matthieu 24.12-24.13 Jérémie 2.2-2.5 Hébreux 6.10-6.11 Philippiens 1.9 1 Thessaloniciens 4.9-4.10
5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Apocalypse 2.16 Apocalypse 3.19 Apocalypse 1.20 Apocalypse 3.2-3.3 Apocalypse 2.19
6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Apocalypse 2.14-2.15 Psaumes 139.21-139.22 2 Chroniques 19.2 Psaumes 26.5 2 Jean 1.9-1.10
7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. Apocalypse 2.17 Apocalypse 2.11 Luc 23.43 Apocalypse 22.14 Genèse 2.9
8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Apocalypse 1.17-1.18 Apocalypse 1.8 Apocalypse 1.11 Apocalypse 2.1
9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Apocalypse 3.9 2 Corinthiens 8.9 Jacques 2.5-2.6 2 Corinthiens 6.10 Romains 2.28-2.29
10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Jacques 1.12 Matthieu 10.22 1 Pierre 5.4 Ephésiens 6.12 Apocalypse 2.9
11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. Apocalypse 20.6 Apocalypse 20.14 Apocalypse 21.8 Apocalypse 2.7 Apocalypse 2.17
12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Apocalypse 1.16 Apocalypse 2.16 Apocalypse 1.11 Apocalypse 19.15 Apocalypse 19.21
13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. 1 Timothée 5.8 2 Timothée 2.12 Apocalypse 2.9-2.10 Actes 22.20 Apocalypse 14.12
14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Apocalypse 2.20 2 Pierre 2.15 Nombres 31.16 Actes 15.29 Jude 1.11
15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Apocalypse 2.6
16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. Apocalypse 2.5 2 Thessaloniciens 2.8 Apocalypse 1.16 Apocalypse 2.12 Actes 17.30-17.31
17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. Apocalypse 3.12-3.13 Apocalypse 2.7 Apocalypse 2.11 Esaïe 65.15 Colossiens 3.3
18 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Apocalypse 1.14-1.15 Apocalypse 1.11 Psaumes 2.7 Jean 1.49 Jean 5.25
19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. 1 Timothée 1.5 2 Thessaloniciens 1.3 2 Pierre 1.7 Colossiens 3.14 Jean 15.2
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Apocalypse 2.14 1 Rois 16.31 Actes 15.29 2 Rois 9.7 1 Corinthiens 10.18-10.21
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Apocalypse 9.20-9.21 2 Pierre 3.9 Romains 2.4-2.5 Apocalypse 16.11 Apocalypse 16.9
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; Apocalypse 17.2 Apocalypse 18.9 Ezéchiel 18.30-18.32 Apocalypse 18.3 Ezéchiel 23.29
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. Romains 8.27 Matthieu 16.27 Psaumes 7.9 Actes 1.24 Jérémie 11.20
24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. Actes 15.28 2 Corinthiens 11.3 2 Corinthiens 2.11 Ephésiens 6.11-6.12 Apocalypse 12.9
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. Apocalypse 3.11 1 Thessaloniciens 5.21 Jean 21.22-21.23 Apocalypse 1.7 Apocalypse 22.7
26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, Apocalypse 3.21 Psaumes 2.8 Apocalypse 20.4 Daniel 7.27 Daniel 7.22
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Apocalypse 12.5 Psaumes 2.8-2.9 Apocalypse 19.15 Esaïe 30.14 Jérémie 19.11
28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. Apocalypse 22.16 2 Pierre 1.19 Luc 1.78-1.79
29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Apocalypse 2.7

Cette Bible est dans le domaine public.