Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 35
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. Psaumes 43.1 Exode 14.25 Actes 5.39 Michée 7.9 Néhémie 4.20
2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie. Esaïe 42.13 Exode 15.3 Deutéronome 32.41-32.42 Psaumes 91.4 Psaumes 7.12-7.13
3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako. Psaumes 51.12 Psaumes 76.10 Luc 2.30 Genèse 49.18 Psaumes 62.7
4 Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya. Psaumes 129.5 Esaïe 37.29 Psaumes 40.14-40.15 Jean 18.6 Matthieu 27.1
5 Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini. Job 21.18 Esaïe 29.5 Psaumes 1.4 Hébreux 11.28 Osée 13.3
6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia. Jérémie 23.12 Psaumes 73.18 Proverbes 4.19 Jérémie 13.16
7 Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu. Psaumes 9.15 Job 18.8 Psaumes 140.5 Psaumes 7.3-7.5 Psaumes 119.85
8 Uharibifu na umpate kwa ghafula, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake. 1 Thessaloniciens 5.3 Matthieu 27.3-27.5 Psaumes 141.9-141.10 2 Samuel 17.23 Esaïe 47.11
9 Na nafsi yangu itamfurahia Bwana, Na kuushangilia wokovu wake. Esaïe 61.10 Psaumes 13.5 Psaumes 9.14 Psaumes 33.21 Luc 1.46-1.47
10 Mifupa yangu yote itasema, Bwana, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye. Exode 15.11 Psaumes 86.8 Psaumes 51.8 Psaumes 18.17 Psaumes 71.19
11 Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua. Psaumes 27.12 Matthieu 26.59-26.60 1 Samuel 25.10 Actes 24.5-24.6 1 Samuel 24.9
12 Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa. Jean 10.32 Jérémie 18.20 Psaumes 38.20 1 Samuel 19.4-19.5 1 Samuel 20.31-20.33
13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu. Job 30.25 Matthieu 10.13 Psaumes 69.10-69.11 Luc 10.6 Esaïe 58.3
14 Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye. 2 Samuel 1.11-1.12 2 Samuel 1.17-1.27 Psaumes 38.6 Genèse 24.67 Luc 19.41-19.42
15 Lakini nikijikwaa hufurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wananipapura wala hawakomi. Psaumes 7.2 Matthieu 27.39-27.44 Psaumes 35.8 Jérémie 20.10 Job 30.1-30.12
16 Kama wenye mzaha wakikufuru karamuni Wananisagia meno. Job 16.9 Lamentations 2.16 Psaumes 37.12 1 Samuel 20.24-20.42 Jean 18.28
17 Bwana, hata lini utatazama? Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao, Na mpenzi wangu na wana-simba. Habakuk 1.13 Psaumes 22.20-22.21 Psaumes 13.1-13.2 Psaumes 6.3 Psaumes 57.4
18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi. Psaumes 40.9-40.10 Hébreux 2.12 Psaumes 117.1-117.2 Psaumes 67.1-67.4 Psaumes 69.30-69.34
19 Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e. Psaumes 69.4 Proverbes 6.13 Psaumes 38.19 Jean 15.25 Psaumes 13.4
20 Maana hawasemi maneno ya amani, Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila. Psaumes 38.12 Psaumes 31.13 Matthieu 26.4 Matthieu 12.24 Psaumes 64.4-64.6
21 Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona. Psaumes 22.13 Psaumes 40.15 Psaumes 70.3 Psaumes 54.7 Luc 11.53-11.54
22 Wewe, Bwana, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami. Exode 3.7 Psaumes 28.1 Psaumes 10.1 Psaumes 38.21 Psaumes 71.12
23 Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu. Psaumes 44.23 Psaumes 7.6 Psaumes 80.2 Psaumes 89.26 Esaïe 51.9
24 Unihukumu kwa haki yako, Ee Bwana, Mungu wangu, Wala wasinisimangize. Psaumes 43.1 Psaumes 35.19 Psaumes 26.1 Psaumes 7.8 2 Thessaloniciens 1.6
25 Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza. Lamentations 2.16 Psaumes 124.3 Psaumes 56.1-56.2 Psaumes 140.8 Psaumes 74.8
26 Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. Psaumes 38.16 Psaumes 132.18 Job 19.5 Job 8.22 Psaumes 40.14-40.15
27 Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake. Psaumes 149.4 Psaumes 70.4 Psaumes 40.16 Jérémie 32.40-32.41 Sophonie 3.17
28 Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa. Psaumes 71.24 Psaumes 145.21 Psaumes 145.5 Psaumes 145.1-145.2 Psaumes 34.1

Cette Bible est dans le domaine public.