Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 21
Bible en Swahili de l’est


Relations entre maîtres et esclaves

1 Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi
Deutéronome 4.14 Deutéronome 6.20 Exode 24.3-24.4 Nombres 35.24 1 Thessaloniciens 4.1
2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Deutéronome 15.18 Deutéronome 15.12-15.15 Néhémie 5.8 Néhémie 5.1-5.5 Jérémie 34.8-34.17
3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.
Deutéronome 15.12-15.14
4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
5 Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru;
2 Corinthiens 5.14-5.15 Deutéronome 15.16-15.17 Esaïe 26.13
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.
Sophonie 3.3 Exode 22.28 Lévitique 25.23 Esaïe 1.26 1 Samuel 8.1-8.2
7 Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo.
Néhémie 5.5 Exode 21.2-21.3
8 Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.
Genèse 28.8 1 Samuel 8.6 Deutéronome 21.11-21.14 Juges 9.19 Job 6.15
9 Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake.
10 Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.
1 Corinthiens 7.1-7.6
11 Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.

Dommages corporels et sanctions

12 Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo.
Genèse 9.6 Lévitique 24.17 Matthieu 26.52 Nombres 35.30-35.31 Nombres 35.16-35.24
13 Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia.
Josué 20.2-20.9 1 Samuel 24.18 Deutéronome 4.41-4.43 1 Samuel 24.4 1 Samuel 24.10
14 Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.
1 Rois 2.28-2.34 Hébreux 10.26 Psaumes 19.13 Deutéronome 27.24 Deutéronome 17.12-17.13
15 Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
1 Timothée 1.9 Deutéronome 21.18-21.21 Deutéronome 27.24 Proverbes 30.11 Proverbes 30.17
16 Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo
Deutéronome 24.7 Exode 22.4 1 Timothée 1.10 Genèse 37.28 Genèse 40.15
17 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
Proverbes 20.20 Proverbes 30.11 Deutéronome 27.16 Matthieu 15.3-15.6 Proverbes 30.17
18 Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake;
Exode 21.20 Exode 2.13 2 Samuel 14.6 Deutéronome 25.11 Exode 21.22
19 atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa.
Zacharie 8.4 2 Samuel 3.29
20 Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa.
Exode 21.26-21.27 Nombres 35.30-35.33 Genèse 4.15 Deutéronome 19.21 Nombres 35.19
21 Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake.
Lévitique 25.44-25.46
22 Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema.
Deutéronome 22.18-22.19 Exode 21.30 Deutéronome 16.18
23 Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai,
Deutéronome 19.21 Nombres 35.31 Lévitique 24.19
24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
Deutéronome 19.21 Matthieu 7.2 Matthieu 5.38-5.40 Apocalypse 16.6 Luc 6.38
25 kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko.
26 Mtu akimpiga mtumwa wake jicho, au jicho la kijakazi chake, na kuliharibu; atamwacha huru kwa ajili ya jicho lake.
Exode 21.20 Ephésiens 6.9 Colossiens 4.1 Psaumes 10.18 Job 31.13-31.15
27 Au akimpiga mtumwa wake jino likang’oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake.
28 Ng’ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng’ombe ataachiliwa.
Exode 21.32 Genèse 9.5-9.6 Lévitique 20.15-20.16
29 Lakini kwamba huyo ng’ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa.
Deutéronome 21.1-21.9
30 Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa.
Exode 21.22 Exode 30.12 Nombres 35.31-35.33 Proverbes 13.8
31 Akiwa ng’ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo.
32 Ng’ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng’ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng’ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe.
Matthieu 26.15 Zacharie 11.12-11.13 Philippiens 2.7 Genèse 37.28 Exode 21.28-21.29
33 Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo,
Proverbes 28.10 Psaumes 9.15 Jérémie 18.20 Psaumes 119.85 Jérémie 18.22
34 mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.
Exode 22.6 Exode 21.29-21.30 Exode 22.14
35 Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya.
36 Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.

Cette Bible est dans le domaine public.