Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 22.6
Bible en Swahili de l’est


1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.Ecclésiaste 7.1 1 Rois 1.47 Hébreux 11.39 Luc 10.20 Actes 7.10
2 Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote wawili.Job 31.15 Proverbes 14.31 Jacques 2.2-2.5 Job 34.19 Proverbes 29.13
3 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.Proverbes 14.16 Proverbes 27.12 Hébreux 11.7 Proverbes 7.7 1 Thessaloniciens 5.2-5.6
4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.Proverbes 21.21 Esaïe 57.15 Proverbes 3.16 Psaumes 112.1-112.3 Esaïe 33.6
5 Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.Proverbes 15.19 1 Jean 5.18 Psaumes 11.6 Job 18.8 Psaumes 18.26-18.27
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.Ephésiens 6.4 2 Timothée 3.15 Genèse 18.19 Psaumes 78.3-78.6 Deutéronome 6.7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.Jacques 2.6 Proverbes 18.23 Jacques 5.4 Esaïe 24.2 Jacques 5.1
8 Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma.Job 4.8 Psaumes 125.3 Osée 10.13 Esaïe 30.31 Esaïe 9.4
9 Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake.Proverbes 19.17 Hébreux 13.16 Psaumes 112.9 2 Corinthiens 9.6-9.11 1 Pierre 4.9
10 Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma.Genèse 21.9-21.10 1 Corinthiens 5.13 Néhémie 13.28 Proverbes 21.24 Psaumes 101.5
11 Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake.Proverbes 16.13 Matthieu 5.8 Psaumes 101.6 Proverbes 14.35 Daniel 3.30
12 Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.Actes 8.9-8.12 Matthieu 16.16-16.18 Apocalypse 11.3-11.11 Esaïe 59.19-59.21 2 Timothée 3.8-3.9
13 Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.Proverbes 15.19 Nombres 13.32-13.33 Proverbes 26.13-26.16
14 Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na Bwana atatumbukia ndani yake.Ecclésiaste 7.26 Proverbes 23.27 Proverbes 6.24-6.29 Juges 16.20-16.21 Néhémie 13.26
15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.Proverbes 13.24 Proverbes 29.15 Proverbes 19.18 Proverbes 23.13-23.14 Jean 3.6
16 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.Jacques 2.13 Psaumes 12.5 Proverbes 28.22 Luc 14.12-14.14 Jacques 5.1-5.5
17 Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu;Proverbes 23.12 Psaumes 90.12 Ecclésiaste 7.25 Proverbes 3.1 Ecclésiaste 8.9
18 maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako.Proverbes 2.10 Jean 7.38 Psaumes 119.162 Proverbes 25.11 Proverbes 16.21
19 Ili matumaini yako uyaweke kwa Bwana, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe.Proverbes 3.5 Jérémie 17.7 1 Pierre 1.21 Esaïe 26.4 Esaïe 12.2
20 Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa;Proverbes 8.6 Osée 8.12 2 Pierre 1.19-1.21 2 Timothée 3.15-3.17 Psaumes 12.6
21 ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli?Luc 1.3-1.4 1 Pierre 3.15 1 Jean 5.13 Jean 20.31
22 Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni;Zacharie 7.10 Malachie 3.5 Exode 23.6 Proverbes 22.16 Job 31.21
23 Kwa sababu Bwana atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka.1 Samuel 25.39 Psaumes 12.5 Proverbes 23.11 Psaumes 140.12 Jérémie 51.36
24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;Proverbes 29.22 Proverbes 21.24 2 Corinthiens 6.14-6.17
25 Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.1 Corinthiens 15.33 Proverbes 13.20 Psaumes 106.35
26 Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu;Proverbes 11.15 Proverbes 17.18 Proverbes 27.13 Proverbes 6.1-6.5
27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?Proverbes 20.16 2 Rois 4.1 Exode 22.26-22.27
28 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako.Deutéronome 19.14 Proverbes 23.10 Deutéronome 27.17 Job 24.2
29 Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.Genèse 41.46 Proverbes 10.4 Matthieu 25.21 2 Timothée 4.2 1 Rois 10.8

Cette Bible est dans le domaine public.