Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 28
Bible en Swahili de l’est


1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Deutéronome 28.7 Psaumes 53.5 1 Thessaloniciens 2.2 Lévitique 26.17 Esaïe 26.3-26.4
2 Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa Genèse 45.5-45.8 Osée 13.11 Daniel 4.27 1 Rois 16.8-16.29 2 Rois 15.8-15.31
3 Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Matthieu 18.28-18.30
4 Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Ephésiens 5.11 Matthieu 3.7 Romains 1.32 1 Rois 18.18 Matthieu 14.4
5 Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote. Psaumes 92.6 Jean 7.17 1 Jean 2.27 1 Jean 2.20 Jacques 1.5
6 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri. Proverbes 19.1 Luc 16.19-16.23 Proverbes 28.18 Proverbes 19.22 Actes 24.24-24.27
7 Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye. 1 Pierre 4.3-4.4 Proverbes 2.1-2.6 Proverbes 29.3 Luc 15.13 Proverbes 19.26
8 Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Proverbes 13.22 Lévitique 25.36 Exode 22.25 Proverbes 14.31 2 Samuel 12.6
9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Psaumes 66.18 Psaumes 109.7 Zacharie 7.11-7.13 Proverbes 15.8 Esaïe 1.15-1.16
10 Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema. Proverbes 26.27 Matthieu 6.33 Psaumes 37.25-37.26 Proverbes 15.6 Galates 2.4
11 Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe; Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana. Ecclésiaste 9.15-9.17 Romains 12.16 Proverbes 26.16 1 Timothée 6.17 Luc 16.13-16.14
12 Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha. Proverbes 29.2 Proverbes 11.10 Proverbes 28.28 Esther 8.15-8.17 1 Rois 18.13
13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Job 31.33 Psaumes 32.3-32.5 1 Jean 1.8-1.10 Jérémie 2.22-2.23 Daniel 9.20-9.23
14 Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara. Proverbes 23.17 Esaïe 66.2 Jérémie 32.40 Psaumes 95.8 Proverbes 29.1
15 Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini. Matthieu 2.16 1 Pierre 5.8 2 Rois 21.16 Exode 1.22 Esther 3.6-3.10
16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake. Esaïe 3.12 Ecclésiaste 4.1 1 Rois 12.10 Exode 18.21 1 Rois 12.14
17 Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. Genèse 9.6 Exode 21.14 Nombres 35.14-35.34 Matthieu 27.4-27.5 2 Chroniques 24.21-24.25
18 Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. Proverbes 10.9 Proverbes 28.6 Psaumes 73.18-73.20 Proverbes 11.3-11.6 1 Thessaloniciens 5.3
19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Proverbes 12.11 Luc 15.12-15.17 Juges 9.4 Proverbes 23.20-23.21 Proverbes 27.23-27.27
20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. Proverbes 20.21 Proverbes 13.11 Luc 16.10-16.12 Proverbes 28.22 Apocalypse 2.10
21 Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate. Ezéchiel 13.19 Proverbes 24.23 Proverbes 18.5 Osée 4.18 Michée 7.3
22 Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia. Proverbes 23.6 Proverbes 28.20 1 Timothée 6.9 Job 20.18-20.22 Genèse 19.17
23 Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake. Proverbes 27.5-27.6 Matthieu 18.15 1 Rois 1.23 2 Samuel 12.7 1 Rois 1.32-1.40
24 Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. Proverbes 18.9 Proverbes 19.26 Matthieu 15.4-15.6 Juges 17.2 Proverbes 28.7
25 Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye Bwana atawandishwa. Proverbes 15.18 Proverbes 11.25 1 Timothée 6.6 Proverbes 13.4 Proverbes 22.10
26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. Proverbes 3.5 Jacques 3.13-3.18 Job 28.28 Jérémie 17.9 2 Rois 8.13
27 Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. Proverbes 19.17 Proverbes 22.9 Deutéronome 15.7 Proverbes 11.26 Psaumes 41.1-41.3
28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka. Proverbes 28.12 Actes 12.23-12.24 Job 24.4 Proverbes 29.2 Esther 8.17

Cette Bible est dans le domaine public.