Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 3
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Proverbes 4.5 Proverbes 1.8 Psaumes 119.16 Jean 14.21-14.24 Jérémie 31.33
2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Proverbes 4.10 Proverbes 9.11 Psaumes 91.16 Psaumes 119.165 1 Timothée 4.8
3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Proverbes 7.3 Proverbes 6.21 2 Corinthiens 3.3 Deutéronome 6.8 Jérémie 17.1
4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Luc 2.52 Psaumes 111.10 1 Samuel 2.26 Romains 14.18 Genèse 39.21
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Psaumes 37.5 Jérémie 17.7-17.8 Proverbes 28.26 Psaumes 37.3 Psaumes 62.8
6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Proverbes 16.3 Psaumes 32.8 Philippiens 4.6 Jérémie 10.23 Jacques 1.5
7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Job 28.28 Proverbes 16.6 Job 1.1 Romains 12.16 Esaïe 5.21
8 Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. Job 21.24 Proverbes 4.22 Psaumes 147.3 Esaïe 1.6 Proverbes 16.24
9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Exode 23.19 Philippiens 4.17-4.18 Exode 22.29 1 Corinthiens 16.2 Exode 34.26
10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya. Deutéronome 28.8 Ecclésiaste 11.1-11.2 Proverbes 11.24-11.25 Joël 2.24 Malachie 3.10-3.11
11 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye. Job 5.17 Hébreux 12.5-12.12 1 Corinthiens 11.32 2 Corinthiens 4.1 Psaumes 94.12
12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. Deutéronome 8.5 Psaumes 103.13 Proverbes 29.17 Apocalypse 3.19 Proverbes 13.24
13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Ecclésiaste 9.15-9.18 Proverbes 4.5-4.9 1 Rois 10.23-10.24 Proverbes 8.32-8.35 1 Rois 10.1-10.9
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Proverbes 8.19 Proverbes 16.16 Proverbes 8.10-8.11 Job 28.13-28.19 Proverbes 2.4
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Proverbes 8.11 Job 28.18 Proverbes 20.15 Matthieu 13.44-13.46 Psaumes 73.25-73.26
16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Proverbes 3.2 Psaumes 21.4 1 Rois 3.13 Proverbes 4.6-4.10 1 Timothée 4.8
17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Psaumes 119.165 Matthieu 11.28-11.30 Luc 1.79 Psaumes 119.103 Psaumes 19.10-19.11
18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye. Genèse 2.9 Proverbes 11.30 Proverbes 13.12 Apocalypse 22.2 Apocalypse 2.7
19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Psaumes 104.24 Psaumes 136.5 Jérémie 10.12 Proverbes 8.27-8.29 Jérémie 51.15
20 Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande. Genèse 7.11 Deutéronome 33.28 Job 38.26-38.28 Genèse 27.28 Job 38.8-38.11
21 Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Josué 1.8 Deutéronome 32.46-32.47 Proverbes 4.21 Deutéronome 6.6-6.9 Hébreux 2.1-2.3
22 Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako. Proverbes 1.9 Proverbes 4.22 Jean 12.49-12.50 Esaïe 38.16
23 Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Proverbes 4.12 Proverbes 10.9 Psaumes 37.31 Psaumes 121.8 Zacharie 10.12
24 Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Psaumes 3.5 Proverbes 6.22 Psaumes 4.8 Jérémie 31.26 Psaumes 127.2
25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. 1 Pierre 3.14 Psaumes 91.5 Esaïe 41.10-41.14 Daniel 3.17-3.18 Esaïe 8.12-8.13
26 Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe. 1 Samuel 2.9 Psaumes 91.3 Habakuk 3.17-3.18 Proverbes 14.26 Psaumes 91.9-91.10
27 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Galates 6.10 Jacques 2.15-2.16 Romains 13.7 Jacques 5.4 Genèse 31.29
28 Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Lévitique 19.13 Ecclésiaste 9.10 1 Timothée 6.18 Ecclésiaste 11.6 Deutéronome 24.12-24.15
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Proverbes 6.14 Psaumes 59.3 Proverbes 16.29-16.30 Proverbes 6.18 Proverbes 14.22
30 Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote. Proverbes 17.14 Proverbes 25.8-25.9 Proverbes 18.6 Matthieu 5.39-5.41 2 Timothée 2.24
31 Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Proverbes 24.1 Psaumes 37.1 Galates 5.21 Proverbes 24.19-24.20 Proverbes 2.12-2.15
32 Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Psaumes 25.14 Proverbes 11.20 Job 29.4 Jean 15.15 Jean 14.21-14.24
33 Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Malachie 2.2 Psaumes 37.22 Psaumes 1.3 Lévitique 26.14-26.46 Zacharie 5.3-5.4
34 Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. 1 Pierre 5.5 Jacques 4.6 Psaumes 138.6 Proverbes 9.12 Esaïe 57.15
35 Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha. Esaïe 65.13-65.15 1 Samuel 2.30 Proverbes 13.8 Proverbes 4.8 Daniel 12.2-12.3

Cette Bible est dans le domaine public.