Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 6
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono, Proverbes 22.26 Proverbes 17.18 Proverbes 11.15 Proverbes 20.16 Job 17.3
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako, Proverbes 18.7 Proverbes 12.13
3 Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako. 2 Samuel 24.14 Exode 10.3 2 Chroniques 36.12 Psaumes 31.8 2 Chroniques 12.5
4 Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia. Psaumes 132.4 Marc 13.35-13.36 Proverbes 6.10-6.11 Ecclésiaste 9.10 Matthieu 24.17-24.18
5 Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego. Psaumes 124.7 Psaumes 91.3 Proverbes 1.17 Psaumes 11.1
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Hébreux 6.12 Proverbes 20.4 Proverbes 10.26 Proverbes 13.4 Matthieu 25.26
7 Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Job 39.26-39.30 Job 41.4-41.34 Job 38.39-39.12 Proverbes 30.27
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Proverbes 10.5 Proverbes 30.25 1 Timothée 6.19
9 Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Proverbes 24.33-24.34 Jérémie 4.14 Romains 13.11 Proverbes 1.22 Psaumes 94.8
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Proverbes 6.6 Proverbes 23.33-23.34 Proverbes 24.33-24.34
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. Proverbes 24.34 Proverbes 10.4 Proverbes 20.4 Proverbes 13.4
12 Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. Proverbes 4.24 Proverbes 16.27 Proverbes 17.4 Actes 20.30 Matthieu 12.34
13 Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake. Psaumes 35.19 Proverbes 10.10 Job 15.12 Proverbes 5.6
14 Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi. Michée 2.1 Proverbes 6.18-6.19 Psaumes 36.4 Proverbes 3.29 Proverbes 22.8
15 Basi msiba utampata kwa ghafula; Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona. Jérémie 19.11 2 Chroniques 36.16 Proverbes 1.27 Psaumes 73.18-73.20 1 Thessaloniciens 5.3
16 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Proverbes 30.18 Proverbes 11.1 Deutéronome 25.16 Proverbes 30.21 Proverbes 11.20
17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Proverbes 12.22 Psaumes 101.5 Esaïe 1.15 Psaumes 120.2-120.3 Psaumes 5.6
18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Genèse 6.5 Proverbes 1.16 Romains 3.15 Zacharie 8.17 Esaïe 59.7
19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu. Psaumes 27.12 Proverbes 19.5 Proverbes 6.14 Proverbes 19.9 Proverbes 25.18
20 Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako. Ephésiens 6.1 Proverbes 30.11 Deutéronome 27.16 Proverbes 1.8-1.9 Proverbes 23.22
21 Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako. Proverbes 3.3 Proverbes 7.3-7.4 2 Corinthiens 3.3 Proverbes 4.6 Deutéronome 6.8
22 Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe. Proverbes 2.11 Proverbes 3.23-3.24 Psaumes 119.24 Psaumes 119.9 Psaumes 119.54
23 Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima. Psaumes 119.105 Psaumes 19.8 Proverbes 15.31 Proverbes 4.4 Proverbes 4.13
24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. Proverbes 5.3 Proverbes 2.16 Proverbes 7.5 Ecclésiaste 7.26
25 Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Matthieu 5.28 2 Rois 9.30 Jacques 1.14-1.15 Esaïe 3.16 2 Samuel 11.2-11.5
26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani Proverbes 29.3 Proverbes 5.10 1 Samuel 2.36 Genèse 39.14 Luc 15.13-15.15
27 Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Osée 7.4-7.7 Jacques 3.5 Job 31.9-31.12
28 Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? 29 Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia. 2 Samuel 11.3-11.4 Jérémie 5.8-5.9 Lévitique 20.10 Genèse 26.10-26.11 Genèse 12.18-12.19
30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; Job 38.39
31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake. Matthieu 18.25 Job 20.18 2 Samuel 12.6 Exode 22.1-22.4 Luc 19.8
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Proverbes 7.7 Genèse 41.39 Genèse 39.9-39.10 Exode 20.14 Hébreux 13.4
33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. Proverbes 5.9-5.11 Psaumes 51.1 Genèse 49.4 Psaumes 51.8 1 Rois 15.5
34 Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi. Proverbes 27.4 Cantique 8.6 Nombres 5.14 1 Corinthiens 10.22 Juges 19.29-19.30
35 Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi. Proverbes 7.13 Proverbes 8.25 Malachie 2.9 2 Rois 5.1 Proverbes 4.3

Cette Bible est dans le domaine public.