Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Jérémie 38.18 Bible en Swahili de l’est
Jérémie dans une citerne
1 Na Shefatia, mwana wa Matani, na Gedalia, mwana wa Pashuri, na Yukali, mwana wa Shelemia, na Pashuri, mwana wa Malkiya, wakayasikia maneno ambayo Yeremia aliwaambia watu wote, kusema, Néhémie 7.9 Actes 4.6-4.10 1 Chroniques 9.12 Jérémie 21.1-21.10 Néhémie 11.12 2 Bwana asema hivi, Akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atokaye kwenda kwa Wakaldayo ataishi, naye atapewa maisha yake yawe kama nyara, naye ataishi. Jérémie 34.17 Jérémie 39.18 Jérémie 45.5 Jérémie 42.17 Ezéchiel 14.21 3 Bwana asema hivi, Bila shaka mji huu utatiwa katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli, naye atautwaa. Jérémie 21.10 Jérémie 32.3-32.5 4 Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari. Jérémie 26.11 Amos 7.10 1 Rois 21.20 Exode 5.4 Néhémie 6.9 5 Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu. 2 Samuel 3.39 2 Samuel 19.22 1 Samuel 15.24 Jean 19.12-19.16 Proverbes 29.25 6 Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. Zacharie 9.11 Jérémie 37.21 Jérémie 37.16 Psaumes 40.2 Actes 16.24 7 Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kama wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini; Jérémie 29.2 Jérémie 37.13 Amos 5.10 Deutéronome 21.19 Jérémie 13.23 8 Ebedmeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akamwambia mfalme, akisema, 9 Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji. Jérémie 52.6 Job 31.34 Proverbes 31.8-31.9 Esther 7.4-7.6 Proverbes 24.11-24.12 10 Ndipo mfalme akamwamuru Ebedmeleki, Mkushi, akisema, Chukua pamoja nawe watu thelathini toka hapa, ukamtoe Yeremia shimoni, kabla hajafa. Proverbes 21.1 Esther 5.2 Esther 8.7 Psaumes 75.10 11 Basi Ebedmeleki akawachukua watu hao pamoja naye, akaingia ndani ya nyumba ya mfalme chini ya ghala, akatoa mle nguo zilizotupwa, na vitambaa vikuukuu, akamtelemshia Yeremia shimoni kwa kamba. 12 Naye Ebedmeleki, Mkushi, akamwambia Yeremia, Tia nguo hizi zilizotupwa, na vitambaa hivi vikuukuu, chini ya kamba kwapani. Naye Yeremia akafanya hivyo. Romains 12.15 Ephésiens 4.32 Romains 12.10 13 Basi wakamwinua Yeremia kwa kamba hizo, wakamtoa shimoni; naye Yeremia akakaa katika uwanda wa walinzi. Jérémie 37.21 Actes 28.30 Actes 28.16 Actes 23.35 1 Rois 22.27