Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 14.35
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.Luc 11.37 Marc 3.2 Luc 20.20 Proverbes 23.7 Psaumes 41.6
2 Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura. 3 Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo?Matthieu 12.10 Matthieu 22.35 Marc 3.4 Luc 6.9 Matthieu 12.2
4 Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake.Matthieu 22.46 Matthieu 21.25-21.27
5 Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?Luc 13.15 Exode 23.4-23.5 Daniel 4.24 Matthieu 12.11-12.12
6 Nao hawakuweza kujibu maneno haya.Luc 20.40 Luc 13.17 Luc 20.26 Actes 6.10 Luc 21.15
7 Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,Luc 11.43 3 Jean 1.9 Matthieu 23.6 Actes 8.18-8.19 Philippiens 2.3
8 Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,Proverbes 25.6-25.7
9 akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.Proverbes 11.2 Esther 6.6-6.12 Proverbes 16.18 Daniel 4.30-4.34 Ezéchiel 28.2-28.10
10 Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.Proverbes 25.6-25.7 Apocalypse 3.9 1 Samuel 15.17 Proverbes 15.33 Esaïe 60.14
11 Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.Luc 18.14 Proverbes 29.23 Matthieu 23.12 Jacques 4.6 1 Pierre 5.5
12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.Jacques 2.1-2.6 Matthieu 5.46 Luc 6.32-6.36 Matthieu 6.1-6.4 Proverbes 22.16
13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,Luc 14.21 Néhémie 8.10 Néhémie 8.12 Deutéronome 14.29 Philémon 1.7
14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.Actes 24.15 Matthieu 6.4 Proverbes 19.17 Matthieu 25.34-25.40 Jean 5.29
15 Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.Apocalypse 19.9 Luc 13.29 Luc 22.30 Matthieu 8.11 Jean 6.27-6.59
16 Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,Matthieu 22.2-22.14 Apocalypse 22.17 Esaïe 55.1-55.7 Luc 14.16-14.24 Apocalypse 3.20
17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.Matthieu 10.1-10.4 Actes 3.24-3.26 Matthieu 11.27-11.29 Proverbes 9.1-9.5 Jean 7.37
18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.1 Timothée 6.9-6.10 Luc 17.26-17.31 Esaïe 28.12-28.13 1 Jean 2.15-2.16 Jean 5.40
19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.1 Corinthiens 7.33 Luc 14.26-14.28 Luc 18.29-18.30 1 Corinthiens 7.29-7.31 Deutéronome 24.5
21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.Luc 14.13 Jean 9.39 Esaïe 33.23 Proverbes 9.3-9.4 Matthieu 11.5
22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.Actes 1.1-1.9 Colossiens 2.9 Jean 14.2 Psaumes 103.6 1 Timothée 2.5-2.6
23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.Actes 13.47-13.48 Esaïe 11.10 Actes 10.44-10.48 Colossiens 1.23 Actes 11.18-11.21
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.Matthieu 21.43 Actes 13.46 Jean 3.19 Proverbes 1.24-1.32 Jean 8.21
25 Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,Jean 6.24-6.27 Luc 12.1
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Matthieu 10.37 Jean 12.25 Philippiens 3.8 Apocalypse 12.11 Actes 20.24
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Matthieu 10.38 Luc 9.23-9.25 Marc 8.34-8.37 2 Timothée 1.12 Actes 14.22
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?Proverbes 24.27 2 Pierre 1.13-1.14 Matthieu 10.22 Matthieu 8.20 1 Thessaloniciens 3.4-3.5
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, 30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.1 Corinthiens 3.11-3.14 Hébreux 6.4-6.8 2 Jean 1.8 Hébreux 10.38 Matthieu 7.27
31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?Proverbes 20.18 2 Rois 18.20-18.22 Proverbes 25.8 1 Rois 20.11
32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.Matthieu 5.25 Actes 12.20 Jacques 4.6-4.10 Luc 12.58 Job 40.9
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Philippiens 3.7-3.8 Luc 5.28 1 Jean 2.15-2.16 Luc 5.11 Luc 18.22-18.23
34 Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?Matthieu 5.13 Colossiens 4.6 Marc 9.49-9.50 Hébreux 2.4-2.8
35 Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.Matthieu 11.15 Apocalypse 2.29 Apocalypse 2.7 Apocalypse 2.11 Luc 8.8

Cette Bible est dans le domaine public.