1 Yoshua akawakusanya kabila zote za Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maakida wao nao wakahudhuria mbele za Mungu.
Josué 23.2 1 Samuel 10.19 Juges 9.1-9.3 Actes 10.33 1 Rois 12.1
2 Yoshua akawaambia watu wote, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng’ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine.
Genèse 31.53 Genèse 31.30 Esaïe 51.2 Josué 24.15 Ezéchiel 16.3
3 Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng’ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka.
Genèse 21.2-21.3 Actes 7.2-7.3 Genèse 12.1-12.4 Genèse 15.5 Psaumes 127.3
4 Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri.
Deutéronome 2.5 Genèse 36.8 Actes 7.15 Genèse 25.24-25.26 Psaumes 105.23
5 Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi.
Exode 3.10 Exode 7.1-7.12 Exode 12.51 Exode 12.37 Exode 4.12-4.14
6 Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanyi mkaifikilia bahari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka bahari ya Shamu.
Exode 12.37 Néhémie 9.11 Psaumes 136.13-136.15 Actes 7.36 Exode 14.1-14.15
7 Nao walipomlilia Bwana, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.
Exode 14.20 Exode 14.27-14.28 Josué 5.6 Deutéronome 29.2 Exode 14.10
8 Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani; nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu.
Nombres 21.21-21.35 Deutéronome 2.32-3.7 Psaumes 135.10-135.11 Psaumes 136.17-136.22 Josué 13.10
9 Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu akamwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani;
Juges 11.25 Nombres 22.2 Michée 6.5 Deutéronome 23.4-23.5 Nombres 22.5-22.21
10 lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu; kwa hiyo akafuliza kuwabarikia ninyi; basi nikawatoa katika mkono wake.
Nombres 22.11-22.12 Nombres 22.18-22.20 Esaïe 54.17 Deutéronome 23.5 Nombres 22.35
11 Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu.
Josué 3.14-3.17 Josué 4.10-4.12 Néhémie 9.24-9.25 Josué 4.23 Actes 7.45
12 Nikatuma mavu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako.
Exode 23.28 Deutéronome 7.20 Psaumes 44.3-44.6
13 Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.
Josué 11.13 Deutéronome 8.7 Deutéronome 6.10-6.12 Proverbes 13.22 Josué 21.45
14 Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana.
Josué 24.23 1 Samuel 12.24 Deutéronome 10.12 Deutéronome 18.13 Ezéchiel 23.3
15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
1 Rois 18.21 Juges 6.10 Exode 23.24 Ruth 1.15-1.16 Jean 6.67-6.68
16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine;
Romains 3.6 1 Samuel 12.23 Romains 6.2 Hébreux 10.38-10.39
17 kwa maana Bwana, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao.
Esaïe 63.7-63.14 Amos 2.9-2.10 Exode 19.4 Deutéronome 32.11-32.12 Josué 24.5-24.14
18 Bwana ndiye aliyewafukuza watu wa mataifa yote watoke mbele yetu, naam, Waamori waliokaa katika nchi hii; basi, kwa sababu hiyo sisi nasi tutamtumikia Bwana, maana yeye ndiye Mungu wetu.
Exode 10.2 Psaumes 116.16 Luc 1.73-1.75 Exode 15.2 Michée 4.2
19 Yoshua akawaambia watu, Hamwezi kumtumikia Bwana; kwa kuwa yeye ni Mungu mtakatifu; yeye ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa yenu, wala dhambi zenu.
Lévitique 19.2 Exode 20.5 Exode 23.21 Psaumes 99.9 Psaumes 99.5
20 Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema.
1 Chroniques 28.9 Actes 7.42 Esaïe 63.10 2 Chroniques 15.2 Esaïe 65.11-65.12
21 Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia Bwana.
Exode 20.19 Exode 24.7 Exode 19.8 Deutéronome 5.27-5.28 Deutéronome 26.17
22 Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua Bwana, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi.
Psaumes 119.173 Psaumes 119.11 Deutéronome 26.17 Luc 19.22 Job 15.6
23 Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa Bwana, Mungu wa Israeli.
Josué 24.14 Osée 14.8 Genèse 35.2-35.4 Hébreux 12.28-12.29 Exode 20.23
24 Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, Bwana, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.
Deutéronome 5.27-5.29 Exode 19.8 Exode 24.7 Exode 24.3
25 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.
Exode 15.25 2 Chroniques 23.16 2 Rois 11.17 Néhémie 9.38 Exode 24.7-24.8
26 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana.
Juges 9.6 Genèse 35.4 Exode 24.4 Genèse 28.18-28.22 Genèse 35.8
27 Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya Bwana aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Josué 22.27-22.28 Luc 19.40 Josué 22.34 Deutéronome 31.21 2 Timothée 2.12-2.13
28 Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake.
Juges 2.6
29 Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, mwenye umri wa miaka mia na kumi.
Juges 2.8 Apocalypse 14.13 Genèse 50.22 Genèse 50.26 Psaumes 115.17
30 Wakamzika katika mpaka wa urithi wake, huko Timnath-sera; ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
Josué 19.50 Juges 2.9 2 Samuel 23.30
31 Nao Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya Bwana, aliyowatendea Israeli.
Juges 2.7 Deutéronome 11.2 Deutéronome 31.13 2 Chroniques 24.2 Actes 20.29
32 Na hiyo mifupa ya Yusufu, ambayo wana wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri, wakaizika huko Shekemu katika ile sehemu ya nchi, Yakobo aliyoinunua kwa wana wa Hamori, babaye Shekemu, kwa vipande mia vya fedha; nayo ikawa ni urithi wa wana wa Yusufu.
Exode 13.19 Genèse 33.19 Genèse 50.25 Actes 7.16 Jean 4.5
33 Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika katika kilima cha Finehasi mwanawe, ambacho alipewa yeye katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Exode 6.25 Josué 22.13 Esaïe 57.1-57.2 Nombres 20.26-20.28 Juges 20.28