Juda et Tamar
1 Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
1 Samuel 22.1 Michée 1.15 2 Rois 4.8 Proverbes 13.20 2 Samuel 23.13
2 Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.
1 Chroniques 2.3 Genèse 24.3 Juges 14.2 Genèse 6.4 Genèse 3.6
3 Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.
Genèse 46.12 Nombres 26.19
4 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.
Genèse 46.12 Nombres 26.19
5 Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.
Nombres 26.20 1 Chroniques 4.21 Genèse 38.26 Genèse 46.12 Genèse 38.11
6 Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.
Matthieu 1.3 Genèse 21.21 Genèse 24.3
7 Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua.
1 Chroniques 2.3 Genèse 46.12 Nombres 26.19 2 Chroniques 33.6 Genèse 19.13
8 Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.
Deutéronome 25.5-25.10 Nombres 36.8-36.9 Ruth 1.11 Matthieu 22.23-22.27 Lévitique 18.16
9 Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
Deutéronome 25.6 Jacques 3.16 Ruth 4.10 Proverbes 27.4 Jacques 3.14
10 Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.
Genèse 46.12 Nombres 11.1 Nombres 26.19 2 Samuel 11.27 Jérémie 44.4
11 Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.
Lévitique 22.13 Ruth 1.11-1.13
12 Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao manyoya kondoo huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.
Josué 15.10 Genèse 24.67 2 Samuel 13.39 Juges 14.1 Josué 15.57
13 Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna, akate manyoya ya kondoo zake.
14 Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe.
Genèse 38.26 Jérémie 3.2 Genèse 24.65 Proverbes 7.12 Ezéchiel 16.25
15 Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.
16 Akamgeukia kando ya njia, akasema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, Utanipa nini, ukiingia kwangu?
Matthieu 26.15 2 Samuel 13.11 1 Timothée 6.10 Ezéchiel 16.33 Deutéronome 23.18
17 Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?
Ezéchiel 16.33 Genèse 38.20 Genèse 38.24-38.25 Luc 16.8 Proverbes 20.16
18 Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya muhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.
Genèse 38.25-38.26 Osée 4.11 Jérémie 22.24 Luc 15.22
19 Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake.
Genèse 38.14 2 Samuel 14.2 2 Samuel 14.5
20 Yuda akapeleka yule mwana-mbuzi kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami, ili aipate rehani mkononi mwa huyo mwanamke lakini hakumkuta.
Lévitique 19.17 2 Samuel 13.3 Genèse 20.9 Juges 14.20 Luc 23.12
21 Akauliza watu wa mahali pale, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.
22 Akamrudia Yuda akasema, Sikumwona; hata na watu wa mahali hapo walisema, Hakuwako kahaba.
23 Yuda akasema, Na aichukue yeye, tusije tukatiwa aibu; tazama, nimempelekea mbuzi huyu, wala hukumkuta.
2 Corinthiens 4.2 Proverbes 6.33 Romains 6.21 Apocalypse 16.15 2 Samuel 12.9
24 Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Lévitique 21.9 Juges 19.2 Osée 3.3 Jérémie 3.6 Ezéchiel 16.28
25 Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.
Genèse 38.18 Genèse 37.32 Romains 2.16 Jérémie 2.26 Apocalypse 20.12
26 Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.
1 Samuel 24.17 1 Pierre 4.2-4.3 Tite 2.11-2.12 Matthieu 3.8 Jean 8.9
27 Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake.
Genèse 25.24
28 Ikawa alipokuwa akizaa, mtoto mmoja akatoa mkono, mzalisha akautwaa uzi mwekundu akaufunga mkononi mwake, huku akisema, Huyu ametoka kwanza.
29 Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka. Akasema, Mbona umepita kwa nguvu wewe? Mambo ya nguvu na yakuandame. Kwa hiyo jina lake likaitwa Peresi.
Genèse 46.12 Nombres 26.20 Matthieu 1.3 1 Chroniques 2.4 Néhémie 11.6
30 Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.
1 Chroniques 9.6 Matthieu 1.3 1 Chroniques 2.4