Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Rois 17
Bible en Swahili de l’est


1 Katika mwaka wa kumi na mbili wa Ahazi mfalme wa Yuda Hoshea mwana wa Ela alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka kenda. 2 Rois 15.30
2 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, ila si kama wafalme wa Israeli waliomtangulia. 2 Chroniques 30.5-30.11 2 Rois 15.18 2 Rois 13.2 2 Rois 3.2 2 Rois 15.9
3 Naye Shalmanesa mfalme wa Ashuru akakwea juu yake, Hoshea akawa mtumishi wake, akampa kodi. Osée 10.14 2 Rois 19.36-19.37 2 Rois 15.29 2 Samuel 8.6 2 Rois 18.31
4 Mfalme wa Ashuru akaona fitina katika huyo Hoshea; kwa maana alikuwa ametuma wajumbe kwa So, mfalme wa Misri, wala hakumletea kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka kwa mwaka; kwa hiyo mfalme wa Ashuru akamfunga, akamtia kifungoni. 2 Rois 25.7 2 Rois 24.20 2 Chroniques 32.11 2 Rois 18.14-18.15 Esaïe 30.1-30.4
5 Ndipo mfalme wa Ashuru akakwea katikati ya nchi yote, akaenda Samaria, akauhusuru miaka mitatu. Osée 13.16 Jérémie 52.4-52.5 2 Rois 25.1-25.3 2 Rois 18.9
6 Katika mwaka wa kenda wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi. Deutéronome 28.64 Osée 13.16 1 Chroniques 5.26 Esaïe 21.2 2 Rois 18.10-18.11
7 Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya Bwana, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine. Josué 23.16 Exode 20.2 Néhémie 9.26 1 Rois 11.4 2 Rois 17.35
8 Wakaziendea sheria za mataifa, ambao Bwana aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya. 2 Rois 16.3 Lévitique 18.3 Deutéronome 18.9 2 Rois 17.19 Deutéronome 12.30-12.31
9 Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma. 2 Rois 18.8 Job 31.27 Osée 12.11 Ezéchiel 8.12 Deutéronome 27.15
10 Wakajisimamishia nguzo na maashera juu ya kila mlima mrefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 1 Rois 14.23 Michée 5.14 2 Rois 16.4 Exode 34.13 Lévitique 26.1
11 wakafukiza uvumba huko katika kila mahali pa juu, kama mataifa walivyofanya, ambao Bwana aliwafukuza mbele yao; wakaunda mambo mabaya, ili wamkasirishe Bwana; Jérémie 44.17 2 Rois 21.6 1 Rois 13.1 Psaumes 78.56-78.58 2 Chroniques 28.25
12 wakatumikia sanamu, ambazo Bwana aliwakataza, akasema, Msitende jambo hili. Deutéronome 12.4 Deutéronome 5.7-5.9 Exode 34.14 Exode 20.3-20.5 Deutéronome 4.23-4.25
13 Pamoja na hayo Bwana aliwashuhudia Israeli, na Yuda, kwa kinywa cha kila nabii, na cha kila mwonaji, akisema, Geukeni, na kuziacha njia zenu mbaya, mkazishike amri zangu na hukumu zangu, sawasawa na ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, nikawapelekea kwa kinywa cha manabii watumishi wangu. 1 Samuel 9.9 Jérémie 18.11 Jérémie 35.15 Jérémie 7.3-7.7 Néhémie 9.29-9.30
14 Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini Bwana, Mungu wao. Deutéronome 31.27 Actes 7.51 Psaumes 106.24 Hébreux 3.7-3.8 Psaumes 78.22
15 Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao Bwana alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao. Deutéronome 12.30-12.31 Deutéronome 32.21 Jérémie 2.5 Romains 1.21-1.23 Jérémie 8.9
16 Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali. 1 Rois 16.31 1 Rois 14.15 1 Rois 12.28 1 Rois 14.23 Deutéronome 4.19
17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 2 Rois 21.6 Deutéronome 18.10-18.12 1 Rois 21.20 2 Rois 16.3 Ezéchiel 23.37
18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake. 1 Rois 11.32 1 Rois 11.13 1 Rois 11.36 Deutéronome 32.21-32.26 1 Rois 12.20
19 Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe. 2 Rois 16.3 1 Rois 14.22-14.23 2 Chroniques 21.13 Jérémie 3.8-3.11 Ezéchiel 16.51-16.52
20 Basi Bwana akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake. 2 Rois 15.29 2 Rois 13.3 Jérémie 6.30 2 Chroniques 28.5-28.6 1 Samuel 15.23
21 Maana aliwatenga mbali Israeli na nyumba ya Daudi; nao wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati kuwa mfalme; Yeroboamu akawavuta Israeli wasimfuate Bwana, akawakosesha kosa kubwa. 1 Rois 11.11 1 Rois 11.31 1 Rois 14.16 1 Rois 12.28-12.30 Exode 32.21
22 Nao wana wa Israeli wakaendelea katika dhambi zote za Yeroboamu alizozifanya; hawakujiepusha nazo; 2 Rois 13.6 2 Rois 10.31 2 Rois 13.11 2 Rois 13.2 2 Rois 15.9
23 hata Bwana akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo. 2 Rois 17.6 2 Rois 17.13 1 Rois 14.16 2 Rois 17.18 2 Rois 18.11-18.12
24 Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. 2 Rois 18.34 2 Rois 17.30-17.31 2 Rois 19.13 Esaïe 10.9 Esaïe 37.13
25 Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana; kwa hiyo Bwana akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. 2 Rois 17.41 2 Rois 17.34 2 Rois 17.32 Jonas 1.9 Ezéchiel 14.21
26 Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. 1 Samuel 8.9 2 Rois 17.27 1 Samuel 10.25 Amos 8.14
27 Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. 1 Rois 13.2 2 Chroniques 11.15 Juges 17.13 1 Rois 12.31
28 Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha Bwana. 1 Rois 12.29-12.32 Matthieu 15.14 Esaïe 29.13
29 Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa. Michée 4.5 1 Rois 12.31 Osée 8.5-8.6 Psaumes 135.15-135.18 1 Rois 13.32
30 Watu wa Babeli wakafanya Sukoth-benothi kuwa mungu wao, watu wa Kutha wakafanya Nergali, watu wa Hamathi wakafanya Ashima, 2 Rois 17.24
31 Waavi wakafanya Nibhazi na Tartaki; nao Wasefarvi wakawaunguza wana wao katika moto kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu. 2 Rois 17.24 2 Rois 17.17 2 Rois 19.37 Deutéronome 12.28 Esdras 4.9
32 Basi hivyo wakamcha Bwana, nao wakijifanyia wengine wao kuwa makuhani wa mahali pa juu, ambao waliwafanyia dhabihu katika nyumba za mahali pa juu. 1 Rois 12.31 2 Rois 17.29 1 Rois 13.33 1 Rois 13.31 2 Rois 23.19
33 Wakamcha Bwana, na kuitumikia miungu yao wenyewe, sawasawa na kawaida za mataifa ambao wao walihamishwa kutoka kwao. 2 Rois 17.41 Luc 16.13 Matthieu 6.24 1 Rois 18.21 Sophonie 1.5
34 Hata siku hii ya leo hufanya sawasawa na kawaida za kwanza; wala hawamwogopi Bwana, wala hawazifuati sheria zao, wala hukumu zao, wala ile torati, wala ile amri Bwana aliyowaamuru wana wa Yakobo, ambaye alimpa jina la Israeli; Genèse 35.10 Genèse 32.28 Esaïe 48.1 2 Rois 17.27-17.28 1 Rois 18.11
35 hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka; Juges 6.10 Deutéronome 4.23-4.27 Exode 20.4-20.5 Exode 34.12-34.17 Josué 23.7
36 ila yeye Bwana, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri kwa nguvu nyingi, na kwa mkono ulionyoshwa, yeye ndiye mtakayemcha, yeye ndiye mtakayemsujudia, yeye ndiye mtakayemtolea sadaka; Exode 6.6 Deutéronome 6.13 Exode 9.15 Lévitique 19.32 Jérémie 32.21
37 na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine. Lévitique 19.37 Deutéronome 31.11 Psaumes 19.8-19.11 Deutéronome 12.32 Deutéronome 31.9
38 Na hilo agano nililofanya nanyi, msilisahau; wala msiche miungu mingine; Deutéronome 4.23 Deutéronome 6.12 Deutéronome 8.14-8.18
39 lakini Bwana, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote. 2 Rois 17.36 Luc 1.50 Matthieu 10.28 Luc 1.74-1.75 Luc 1.71
40 Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza. Jérémie 13.23 2 Rois 17.34 2 Rois 17.8 2 Rois 17.12 Deutéronome 4.28
41 Basi mataifa hawa wakamcha Bwana, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo. Sophonie 1.5 Matthieu 6.24 2 Rois 17.32-17.33 1 Rois 18.21 Apocalypse 3.15-3.16

Cette Bible est dans le domaine public.