Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 4.19
Bible en Swahili de l’est


1 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. 2 Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. 3 Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi; 4 na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu. 5 Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. 6 Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. 7 Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. 8 Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu. 9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba. 11 Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni. 12 Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka. 13 Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi. 14 Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye bonde la Wakarashi; kwani hao walikuwa mafundi. 15 Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi. 16 Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli. 17 Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa. 18 Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa. 19 Na wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka. 20 Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi. 21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa mbari ya wafuma nguo za kitani safi, wa mbari ya Ashbea; 22 na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. Na taarifa hizi ni za zamani sana. 23 Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake. 24 Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli; 25 na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma. 26 Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei. 27 Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda. 28 Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali; 29 na huko Bilha, na Esemu, na Toladi; 30 na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi; 31 na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hata wakati wa kumiliki Daudi. 32 Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano, 33 na vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo. 34 Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia; 35 na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli; 36 na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya; 37 na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya; 38 hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na mbari za baba zao zikaongezeka sana. 39 Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo zao malisho. 40 Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu. 41 Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao. 42 Na baadhi yao, maana ya hao wana wa Simeoni, watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi. 43 Nao wakawapiga mabaki ya Waamaleki waliookoka, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.

Cette Bible est dans le domaine public.