Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 20.22
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,Job 2.11 Job 11.1 Job 42.9
2 Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.Romains 10.2 Psaumes 39.2-39.3 Marc 6.25 Jacques 1.19 Job 20.3
3 Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.Job 27.11 Job 20.2 Psaumes 78.2-78.5 Job 19.3 Job 19.29
4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,Psaumes 115.16 Job 15.10 Job 8.8-8.9 Genèse 1.28 Genèse 9.1-9.3
5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?Psaumes 37.35-37.36 Exode 15.9-15.10 Job 15.29-15.34 Galates 6.4 Esther 7.10
6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;Esaïe 14.13-14.14 Abdias 1.3-1.4 Genèse 11.4 Daniel 4.22 Matthieu 11.23
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?Job 14.10 1 Rois 14.10 Psaumes 83.10 2 Rois 9.37 Job 8.18
8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,Psaumes 73.20 Psaumes 90.5 Esaïe 29.7-29.8 Job 18.18 Job 27.21-27.23
9 Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena.Job 7.8 Job 7.10 Job 8.18 Psaumes 37.36 Psaumes 37.10
10 Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake.Job 20.18 Job 27.16-27.17 Job 5.4 Psaumes 109.10 Proverbes 6.31
11 Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini.Job 21.26 Job 13.26 Psaumes 25.7 Ezéchiel 24.13 Proverbes 5.22-5.23
12 Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake;Job 15.16 Psaumes 10.7 Psaumes 109.17-109.18 Genèse 3.6 Ecclésiaste 11.9
13 Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake;Marc 9.43-9.49 Matthieu 5.29-5.30 Nombres 11.18-11.20 Romains 8.13
14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.Proverbes 23.20-23.21 Proverbes 23.29-23.35 Deutéronome 32.24 Proverbes 1.31 2 Samuel 11.2-11.5
15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.Proverbes 23.8 Matthieu 27.3-27.4
16 Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua.Romains 3.13 Actes 28.3-28.6 Matthieu 3.7 Deutéronome 32.24 Esaïe 30.6
17 Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.Deutéronome 32.13-32.14 Job 29.6 Esaïe 41.17 Esaïe 7.22 Esaïe 7.15
18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.Job 20.10 Job 20.15 Matthieu 23.13 Job 31.29 Jérémie 22.17
19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.Job 35.9 Proverbes 14.31 Jacques 2.6 Job 18.15 Jacques 2.13
20 Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia.Ecclésiaste 5.13-5.14 Esaïe 57.20-57.21
21 Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.Job 18.19 Luc 16.24-16.25 Job 15.29 Jérémie 17.11
22 Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia.Apocalypse 18.7 Job 18.7 2 Rois 24.2 Job 1.17 Job 16.11
23 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.Psaumes 78.30-78.31 Nombres 11.33 Genèse 19.24 Malachie 2.2 Psaumes 11.6
24 Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili.Amos 5.19 Esaïe 24.18 2 Samuel 22.35 1 Rois 20.30 Amos 9.1-9.3
25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake.Job 16.13 Job 18.11 Deutéronome 32.41 Psaumes 7.12 2 Samuel 18.14
26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.Psaumes 21.9 Psaumes 120.4 Psaumes 109.9-109.15 Jude 1.13 Esaïe 14.20-14.22
27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake.Esaïe 26.21 Job 16.18 Psaumes 44.20-44.21 Romains 2.16 Malachie 3.5
28 Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.Job 21.30 Proverbes 11.4 Apocalypse 18.17 Job 27.14-27.19 Sophonie 1.18
29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu.Job 27.13 Job 31.2-31.3 Job 18.21 Deutéronome 29.20-29.28 Matthieu 24.51

Cette Bible est dans le domaine public.