Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 21
Bible en Swahili de l’est


1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo. Proverbes 16.9 Proverbes 20.24 Esdras 6.22 Actes 7.10 Daniel 4.35
2 Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huipima mioyo. Proverbes 16.2 Proverbes 16.25 Luc 16.15 1 Samuel 16.7 Proverbes 24.12
3 Kutenda haki na hukumu Humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka. 1 Samuel 15.22 Proverbes 15.8 Osée 6.6 Michée 6.6-6.8 Esaïe 1.11-1.17
4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi. Proverbes 6.17 Esaïe 3.16 Proverbes 15.8 Psaumes 10.4 1 Pierre 5.5
5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Proverbes 10.4 Proverbes 13.4 Proverbes 14.29 Proverbes 27.23-27.27 Proverbes 28.22
6 Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti. Proverbes 20.21 Proverbes 13.11 Proverbes 10.2 2 Pierre 2.3 Proverbes 8.36
7 Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali; Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu. Jérémie 7.15 Proverbes 21.21 Ezéchiel 22.13-22.14 Jérémie 7.9-7.11 Proverbes 10.6
8 Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa. Proverbes 2.15 Tite 3.5 Psaumes 14.2-14.3 Job 15.14-15.16 1 Jean 3.3
9 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi. Proverbes 19.13 Proverbes 25.24 Proverbes 21.19 Proverbes 27.15-27.16 Proverbes 12.4
10 Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu; Jirani yake hapati fadhili machoni pake. Proverbes 3.29 Michée 3.2-3.3 Marc 7.21-7.22 Psaumes 112.9 1 Samuel 25.8-25.11
11 Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima; Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa. Proverbes 19.25 Actes 5.5 Hébreux 2.1-2.3 Proverbes 15.14 Proverbes 9.9
12 Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya; Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia. Psaumes 37.35-37.36 1 Corinthiens 10.5 Job 27.13-27.23 Job 21.28-21.30 Psaumes 107.43
13 Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. Jacques 2.13-2.16 Néhémie 5.1-5.5 Esaïe 1.15-1.17 Matthieu 7.2 Deutéronome 15.7-15.11
14 Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali. Proverbes 18.16 Proverbes 19.6 Proverbes 17.8 1 Samuel 25.35 Genèse 32.20
15 Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. Proverbes 10.29 Psaumes 119.16 Proverbes 21.12 Job 29.12-29.17 Romains 7.22
16 Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa. Psaumes 49.14 Psaumes 125.5 Proverbes 7.26-7.27 Proverbes 2.18-2.19 Proverbes 13.20
17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri. Proverbes 23.21 Proverbes 21.20 1 Timothée 5.6 Luc 15.13-15.16 2 Timothée 3.4
18 Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki; Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili. Proverbes 11.8 Esaïe 55.8-55.9 1 Pierre 3.18 Esaïe 43.3-43.4 Esaïe 53.4-53.5
19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi. Proverbes 21.9 Psaumes 120.5-120.6 Jérémie 9.2 Psaumes 55.6-55.7
20 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza. Psaumes 112.3 Matthieu 25.3-25.4 Proverbes 10.22 Ecclésiaste 5.19 Ecclésiaste 7.11
21 Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima. Matthieu 5.6 Proverbes 15.9 1 Corinthiens 15.58 Esaïe 51.1 1 Timothée 6.11
22 Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu; Na kuziangusha nguvu za tumaini lao. Ecclésiaste 7.19 Proverbes 24.5 2 Samuel 5.6-5.9 2 Samuel 20.16-20.22 Ecclésiaste 9.13-9.18
23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu. Proverbes 12.13 Proverbes 13.3 Proverbes 18.21 Jacques 1.26 Proverbes 17.27-17.28
24 Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake. Psaumes 1.1 Proverbes 1.22 Esther 3.5-3.6 Proverbes 19.29 Proverbes 18.12
25 Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi. Proverbes 13.4 Proverbes 24.30-24.34 Proverbes 19.24 Proverbes 26.16 Proverbes 22.13
26 Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa; Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi. Psaumes 37.26 Psaumes 112.9 1 Thessaloniciens 2.5-2.9 2 Corinthiens 9.9-9.14 Ephésiens 4.28
27 Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya! Esaïe 66.3 Proverbes 15.8 Jérémie 6.20 Amos 5.21-5.22 Psaumes 50.8-50.13
28 Shahidi wa uongo atapotea; Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo. Proverbes 19.5 Proverbes 19.9 Proverbes 12.19 Actes 12.15 2 Corinthiens 1.17-1.20
29 Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu; Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake. Proverbes 11.5 Psaumes 119.59 Jérémie 8.12 Aggée 1.5 Aggée 2.15
30 Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya Bwana. Actes 5.39 Esaïe 8.9-8.10 Proverbes 19.21 Esaïe 14.27 Jérémie 9.23
31 Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini Bwana ndiye aletaye wokovu. Esaïe 31.1 Psaumes 20.7 Psaumes 3.8 Psaumes 33.17-33.18 Psaumes 147.10

Cette Bible est dans le domaine public.