Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 5
Bible en Swahili de l’est


1 Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana; Psaumes 80.8 Luc 20.9 Matthieu 21.33 Marc 12.1 Jérémie 2.21
2 Akafanya handaki kulizunguka pande zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibu-mwitu. Marc 11.13 Jérémie 2.21 Exode 33.16 Matthieu 21.19 Luc 13.6-13.7
3 Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. Psaumes 50.4-50.6 Romains 2.5 Michée 6.2-6.3 Matthieu 21.40-21.41 Psaumes 51.4
4 Je! Ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? Matthieu 23.37 Jérémie 6.29-6.30 Ezéchiel 24.13 2 Chroniques 36.14-36.16 Michée 6.3-6.4
5 Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa; Esaïe 28.18 Lamentations 1.15 Luc 21.24 Esaïe 28.3 Esaïe 10.6
6 nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake. Esaïe 7.23-7.25 Esaïe 24.1-24.3 Jérémie 25.11 2 Chroniques 36.19-36.21 Lévitique 26.33-26.35
7 Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio. Psaumes 80.8-80.11 Matthieu 3.8-3.10 1 Corinthiens 6.8-6.11 Esaïe 58.6-58.8 1 Jean 3.7-3.8
8 Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi! Michée 2.2 Habakuk 2.9-2.12 Jérémie 22.13-22.17 1 Rois 21.16-21.20 Ezéchiel 11.15
9 Bwana wa majeshi asema katika masikio yangu, Hakika majumba mengi yatakuwa ukiwa, naam, majumba makubwa, mazuri, yatakuwa hayana watu. Matthieu 23.38 Esaïe 22.14 Amos 6.11 Amos 3.7 Esaïe 5.6
10 Kwa maana shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu. Lévitique 26.26 Lévitique 27.16 Aggée 2.16 Joël 1.17 Aggée 1.6
11 Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Proverbes 23.29-23.30 Esaïe 5.22 Ecclésiaste 10.16-10.17 Romains 13.13 Proverbes 20.1
12 Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Psaumes 28.5 Job 34.27 Daniel 5.23 Daniel 5.1-5.4 Amos 6.4-6.6
13 Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana. Osée 4.6 Esaïe 1.3 Esaïe 27.11 Esaïe 1.7 Lamentations 4.9
14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. Habakuk 2.5 Apocalypse 20.13-20.15 Luc 21.34 Actes 12.21-12.23 Psaumes 55.15
15 Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa, Esaïe 2.11 Esaïe 2.9 Daniel 4.37 Jérémie 5.9 Esaïe 37.29
16 bali Bwana wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki. Psaumes 46.10 1 Pierre 2.15 Esaïe 29.23 Esaïe 33.5 Esaïe 12.4
17 Ndipo wana-kondoo watakapolisha kama katika malisho yao wenyewe, na mahali pao waliowanda, palipoachwa ukiwa, wageni watakula. Sophonie 2.6 Esaïe 7.25 Sophonie 2.14 Esaïe 17.2 Deutéronome 32.15
18 Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari! Jérémie 23.14 Jérémie 23.10 Psaumes 94.5-94.11 Ezéchiel 13.10-13.11 Jérémie 28.15-28.16
19 Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona. Ezéchiel 12.22 Jérémie 23.36 Jérémie 17.15 Ezéchiel 12.27 Esaïe 66.5
20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu! Proverbes 17.15 Job 17.12 Luc 11.34-11.35 2 Timothée 3.1-3.5 Matthieu 6.22-6.23
21 Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe! Proverbes 3.7 Romains 12.16 1 Corinthiens 3.18-3.20 Romains 11.25 Job 11.12
22 Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo; Esaïe 5.11 Esaïe 28.7 Habakuk 2.15 Esaïe 56.12 Proverbes 23.19-23.20
23 wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake! Esaïe 10.2 Jacques 5.6 Psaumes 94.21 Michée 3.11 Michée 7.3
24 Kwa hiyo kama vile mwali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika mwali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli. Job 18.16 Joël 2.5 Esaïe 30.12 Exode 15.7 Esaïe 30.9
25 Kwa sababu hiyo hasira ya Bwana imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Esaïe 9.21 Esaïe 9.17 Esaïe 10.4 2 Rois 9.37 Jérémie 4.24
26 Naye atawatwekea bendera mataifa toka mbali, Naye atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana. Zacharie 10.8 Esaïe 7.18 Deutéronome 28.49 Esaïe 18.3 Esaïe 11.12
27 Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa; Hakuna asinziaye wala kulala usingizi; Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea. Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika; Job 12.18 Joël 2.7-2.8 Esaïe 45.1 Deutéronome 32.25 Job 12.21
28 Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli; Psaumes 45.5 Jérémie 5.16 Ezéchiel 21.9-21.11 Nahum 2.3-2.4 Esaïe 21.1
29 Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wana-simba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa. Esaïe 42.22 Esaïe 49.24-49.25 Michée 5.8 Zacharie 11.3 Jérémie 50.17
30 Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake. Esaïe 8.22 Joël 2.10 Jérémie 4.23-4.28 Jérémie 6.23 Luc 21.25-21.26

Cette Bible est dans le domaine public.