Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 20.15
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia bara ya Sini, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko.Nombres 13.21 Exode 15.20 Nombres 33.36 Nombres 26.59 Nombres 27.14
2 Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni.Nombres 16.19 Nombres 16.42 Exode 15.23-15.24 Nombres 21.5 Exode 16.7
3 Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za Bwana!Exode 17.2 Nombres 16.31-16.35 Nombres 16.49 Nombres 11.1 Job 3.10-3.11
4 Mbona mmewaleta kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu?Exode 17.3 Exode 5.21 Actes 7.35 Actes 7.39-7.40 Nombres 16.41
5 Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa.Nombres 16.14 Jérémie 2.2 Néhémie 9.21 Ezéchiel 20.36 Jérémie 2.6
6 Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea.Nombres 14.5 Nombres 16.45 Nombres 16.4 Nombres 16.22 Nombres 16.19
7 Bwana akasema na Musa, akinena, 8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.Exode 4.17 Esaïe 43.20 Exode 17.5-17.6 Esaïe 41.17-41.18 Nombres 21.18
9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru.Nombres 17.10
10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?Psaumes 106.32-106.33 Ephésiens 4.26 Genèse 41.16 Romains 15.17-15.19 Actes 3.12-3.16
11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.1 Corinthiens 10.4 Nombres 20.8 Deutéronome 8.15 Exode 17.6 1 Samuel 15.19
12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.Deutéronome 1.37 Nombres 27.14 Nombres 20.24 Ezéchiel 20.41 Ezéchiel 36.23
13 Maji haya ni maji ya Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na Bwana, naye alijionyesha kuwa mtakatifu kati yao.Exode 17.7 Psaumes 95.8 Deutéronome 33.8 Deutéronome 32.51 Esaïe 5.16
14 Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;Juges 11.16-11.17 Deutéronome 23.7 Exode 18.8 Deutéronome 2.4-2.25 Genèse 36.31-36.39
15 jinsi baba zetu walivyotelemkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mwingi, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia;Deutéronome 26.6 Genèse 46.6 Exode 12.40 Genèse 15.13 Actes 7.15
16 tena tulipomlilia Bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho;Exode 14.19 Exode 33.2 Exode 23.20 Exode 6.5 Exode 2.23-2.24
17 tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kuume, wala upande wa kushoto, hata tutakapopita mpaka wako.Deutéronome 2.27 Nombres 21.22-21.24 Deutéronome 2.1-2.4 Deutéronome 2.29 Nombres 21.1
18 Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga. 19 Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lo lote.Deutéronome 2.28 Deutéronome 2.6 Exode 12.38
20 Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu.Juges 11.17 Amos 1.11 Ezéchiel 35.5-35.11 Juges 11.20 Abdias 1.10-1.15
21 Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha.Juges 11.18 Deutéronome 2.29 Deutéronome 23.7 Deutéronome 2.27 Juges 11.24
22 Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikilia mlima wa Hori.Nombres 20.14 Nombres 20.1 Nombres 21.4 Nombres 33.36-33.38 Ezéchiel 47.19
23 Bwana akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia,Nombres 33.37
24 Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.Deutéronome 32.50 Genèse 25.8 Nombres 31.2 Nombres 27.13 Juges 2.10
25 Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori;Nombres 33.38-33.39
26 umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko.Nombres 20.24 Hébreux 7.23-7.24 Esaïe 22.21-22.22 Exode 29.29-29.30 Hébreux 7.11
27 Musa akafanya kama Bwana alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote. 28 Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake, akamvika mwanawe Eleazari mavazi hayo; Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani.Deutéronome 10.6 Exode 29.29-29.30 1 Chroniques 22.11-22.12 Actes 20.25-20.29 1 Chroniques 28.5-28.9
29 Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolea.Deutéronome 34.8 Actes 8.2 2 Chroniques 35.24-35.25 Genèse 1.10

Cette Bible est dans le domaine public.