Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 4
Bible en Swahili de l’est


1 Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, Luc 22.4 Actes 6.12 Actes 5.26 Actes 5.24 Jean 15.20
2 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu. Actes 17.18 1 Thessaloniciens 4.13-4.14 1 Corinthiens 15.12-15.20 Actes 19.23 1 Corinthiens 15.23
3 Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. Actes 5.18 Actes 6.12 Luc 22.52 Luc 22.54 Actes 8.3
4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano. Actes 2.41 Philippiens 1.12-1.18 2 Corinthiens 2.14-2.17 Esaïe 53.12 Jean 12.24
5 Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, Actes 4.8 Michée 2.1 Marc 15.1 Actes 5.34 Luc 23.13
6 na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu. Luc 3.2 Matthieu 26.3 Jean 18.24 Jean 18.13-18.14 Jean 11.49
7 Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? Matthieu 21.23 Exode 2.14 Marc 11.28 Actes 4.10 1 Rois 21.12-21.14
8 Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, Actes 2.4 Actes 7.55 Matthieu 10.19-10.20 Actes 4.5 Luc 12.11-12.12
9 kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, Actes 3.7 Jean 10.32 1 Pierre 4.14 1 Pierre 3.15-3.17 Jean 7.23
10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Actes 3.6 Matthieu 27.63-27.66 Actes 5.29-5.32 Actes 2.36 Daniel 3.18
11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Psaumes 118.22-118.23 Esaïe 28.16 Proverbes 28.1 Matthieu 21.42-21.45 Marc 9.12
12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Apocalypse 20.15 Jean 14.6 Matthieu 1.21 Jean 3.36 1 Corinthiens 3.11
13 Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. 1 Corinthiens 1.27 Matthieu 11.25 Jean 7.15 Actes 2.7-2.12 Jean 18.16-18.17
14 Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Actes 4.10 Actes 4.16 Actes 19.36 Actes 3.8-3.12 Actes 4.21
15 Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, Actes 5.34-5.42 Matthieu 5.22 Actes 26.30-26.32
16 wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. Daniel 8.8 Actes 6.10 Daniel 8.5 Matthieu 27.16 Actes 3.7-3.10
17 Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Actes 5.28 Michée 2.6-2.7 Jérémie 29.25-29.32 Romains 15.18-15.22 Amos 2.12
18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Actes 5.40 Luc 24.46-24.48 Actes 1.8 Actes 5.20
19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; Actes 5.29 Exode 1.17 1 Timothée 2.3 Daniel 3.18 Matthieu 22.21
20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Actes 22.15 Jérémie 20.9 Actes 5.32 Ezéchiel 3.11 Nombres 22.38
21 Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka; Actes 5.26 Luc 20.19 Luc 22.2 Matthieu 9.8 Matthieu 21.46
22 maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini. Actes 9.33 Matthieu 9.20 Jean 9.1 Jean 5.5 Actes 3.2
23 Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. Actes 12.11-12.12 Psaumes 119.63 Actes 2.44-2.46 Psaumes 16.3 Actes 1.13-1.14
24 Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; Néhémie 9.6 Jérémie 32.17 Jérémie 20.13 Actes 16.25 Luc 6.11-6.12
25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili? Actes 1.16 Psaumes 2.1-2.6 Actes 2.30
26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Psaumes 2.2 Psaumes 83.2-83.8 Apocalypse 11.15 Actes 10.38 Hébreux 1.9
27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, Actes 4.30 Matthieu 27.2 Jean 1.11 Matthieu 23.37 Luc 13.31-13.33
28 ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Actes 2.23 Esaïe 46.10 Genèse 50.20 Actes 3.18 Luc 22.22
29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, Actes 4.31 Actes 4.13 Philippiens 1.14 Actes 14.3 Actes 9.27
30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Actes 4.27 Actes 3.6 Jérémie 20.11-20.12 Actes 5.15-5.16 Actes 6.8
31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Actes 2.4 Actes 2.2 Esaïe 65.24 Matthieu 21.22 Jacques 1.5
32 Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 1 Corinthiens 1.10 Ephésiens 4.2-4.6 Philippiens 2.1-2.2 Jean 17.21-17.23 2 Corinthiens 13.11
33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Actes 1.22 Actes 1.8 Jean 1.16 Luc 2.52 Actes 2.32-2.33
34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, Actes 2.45 1 Thessaloniciens 4.12 Luc 22.35 1 Timothée 6.19 Psaumes 34.9-34.10
35 wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Actes 5.2 Actes 2.45 Actes 4.37 2 Corinthiens 8.20-8.21 Actes 6.1-6.6
36 Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, 1 Corinthiens 9.6 Galates 2.1 Actes 12.25-13.1 Actes 15.39 Marc 3.17
37 alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. Matthieu 19.29 Actes 4.34-4.35 Actes 5.1-5.2

Cette Bible est dans le domaine public.